Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Tanzania iko mstari sahihi, utekelezaji wa SDGs- Moshi

Utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs uko katika mstari sahihi nchini Tanzania kufuatia sera mpya zilizopo za kuhakikisha ulinzi wa mapato ya kitaifa kwa mujibu wa Celestine Moshi, mkurugenzi, idara ya ushrikiano wa kimataifa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, akizungumza na Grace Kaneiya wa idhaa hii kandoni mwa mkutano wa viongozi wa ngazi ya juu kuhusu utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs unaondelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Silaha za nyuklia ni mwiba unaopaswa kutolewa

Silaha za nyuklia zimekuwa mwiba kwa wakazi wa dunia hii hasa kwa wale ambao silaha hizo zimetumika na kuwaletea madhara, mathalani huko Hiroshima na Nagasaki nchini Japan. Madhara kama vile watoto kuzaliwa na ulemavu wa viungo, wanawake kushindwa kubeba ujauzito ni miongoni mwa madhara lukuki yaliyosababisha Umoja wa Mataifa kupitia nchi wanachama wake kukutana kwenye makao makuu jijini New York, Marekani kwa takribani wiki tatu kuanzia katikati ya mwezi Juni mwaka huu na hatimaye kupitisha mkataba wa kutokomeza silaha hizo.

Mradi wa nishati ya jua wabadili maisha ya wakaazi Tanzania

Upatikanaji wa huduma ya maji ni changamoto katika nchi nyingi hususan zilizo barani Afrika. Hata hivyo jamii, serikali na mashirika mbalimbali yakiwemo ya Umoja wa Mataifa kama vile benki ya dunia yanachukua hatua ili kupunguza adha hiyo.

Nchini Tanzania waakazi wa mkoa wa Manyara wamepata muorubaini dhidi ya ukosefu wa maji na magonjwa yanayotokana na maji yasiyo safi na salama kufuatia kuanzishwa kwa mradi wa nishati ya jua wa kupampu maji ya bomba. Basi ungana na Joseph Msami katika Makala ifuatayo.

Utalii unatoa fursa za kipato kwa wengi ikiwemo wakulima- UNCTAD

Utalii ni moja ya sekta ambazo inachangia mapato ya nchi huku ikielezwa kuwa mapato yatokanayo na sekta hiyo yameongezeka kutoka dola bilioni 69 kati ya mwaka 1995-1998 hadi dola bilioni 196 kati ya mwaka 2011-2014.

Aidha nchi barani Afrika ni wanufaika wa sekta hii ambayo inatoa fursa za ajira za moja kwa moja katika sekta ya utalii na pia kwa wakulima kwa mfano nchini Tanzania. Basi ungana na Assumpta Massoi wa Idhaa hii katika mahojiano yake na Jane Muthambi, afisa uchumi wa UNCTAD kitengo cha Afrika.

Mbio zatumika Sudan Kusini kujenga maelewano baina ya jamii

Miaka sita ya uhuru wa Sudan Kusini ikitimu tarehe Tisa mwezi huu wa Julai, matumaini ya wananchi kuwa watakuwa na ustawi wa kudumu bado yako mashakani kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo tangu mwezi disemba mwaka 2013.

Bado mamia ya watu ni wakimbizi wa ndani na wengine wanakimbilia nchi jirani, jamii mbali mbali zikiendelea kufarakana. Hata hivyo Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau wake wameamua kutumia mbinu mbali mbali ili kuleta jamii pamoja na miongoni mwao mbinu hizo inasimuliwa na Selina Jerobon kupitia makala hii.

Sauli aeleza ndoto zake za kubadlisha maisha ya vijana na jamii Tanzania

Umoja wa Mataifa hivi sasa unapigia chepuo ushirikishaji wa vijana katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Malengo hayo ni mtambuka ambapo vijana wanaweza kushiriki katika kufanikisha malengo yote iwapo watajiongeza. Mathalani huko Tanzania kijana mmoja amejiongeza na kupigia chepuo lengo namba nne la linalotaka elimu jumuishi na yenye usawa. Kijana huyo Saul Mwame wa kidato cha nne katika shule ya sekondari DCM Mvumi, Dodoma hajasubiri usaidizi bali amejipa changamoto na kuanza kusonga mbele kama anavyotanabaisha katika mahojiano yake na Joseph Msami.

Picha: UNHCR/Video capture

Sanaa yaleta nuru na kujiamini kwa wakimbizi Kakuma

Nchini Kenya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeibuka na mbinu mpya ya kuwezesha wakimbizi kuondokana na tabia ya baadhi ya watu kuwaona wao si binadamu kwa kuwa ni wakimbizi. Mbinu hiyo ilibuniwa na mwanamuziki mashuhuri nchini humo na sasa inaleta siyo tu nuru kwa wakimbizi bali pia kujiamini na kujitambua. je ni nini kinafanyika? Ungana basi na Grace Kaneiya kwenye makala hii.

UNAMID yasaidia kuzima moto Korma, Darfur

Nchini Sudan katika jimbo la Darfur, walinda amani wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, UNAMID waliwezesha kuepusha janga zaidi baada ya kushiriki kuzima moto katika kijiji cha Korma.

Hivi sasa wakazi wa eneo hilo kwa usaidizi wa UNAMID wanajaribu kurejea katika maisha ya kawaida baada ya kunusurika na zahma hiyo. Je nini kilitokea? Jumbe Omari Jumbe wa radio ya ujumbe huo wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, UNAMID anasimulia kwenye makala hii.

Nilitembea kutwa kucha na wanangu kutoka Sudan Kusini hadi Uganda kunusuru maisha-Sehemu ya 2

Kutana na Jade Kide katika sehemu ya pili ya mahojiano na John Kibego.  Yeye ni mama wa watoto wanne na amehaha kusaka hifadhi na kujikuta akitembea usiku na mchana kutoka Sudan Kusini kukimbia machafuko.

Amewasili Uganda katika kambi ya wakimbizi ya Kiryandongo, akiwa ametokea jimboni Equatoria Mashariki nchini Sudan Kusini. Anasilimulia kadhia zinazomakabili akikumbuka namna alivyompoteza mwanae na wazazi kufuatia mgogoro nchini mwake.