Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Fursa na vikwazo katika juhudi za vijana kujikwamua nchini DRC 1

Katika mfululizo wa makala zinazomulika juhudi za vijana katika kujikwamua kiuchumi, tunakupeleka Afrika Mashariki kusikiliza mahojiano na  kijana mjasiriamali Kiiza Serugendo Elwa kutoka mji wa Kiwanja, Jimboni Kivu ya Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Ungana na John Kibego katika sehemu hii ya kwanza ya mahojiano na kijana huyu ambaye kwa sasa yuko nchini Uganda.

(MAHOJIANO)

Kaa chonjo kusikiliza sehemu ya pili ya makala haya juma lijalo.

Picha: UNDP/Kenya_Video capture

Mradi wa UNDP umewapa ujasiri sambamba na kuwawezesha wanawake wa Kimasaai

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Kenya kwa ushirikiano na serikali ya nchi hiyo wameanzisha mradi kwa ajili ya kuwezesha jamii zinazoishi kusini magharibi mwa Kenya karibu na mbuga ya wanyama ya Amboseli. Miradi hiyo inayolenga jamii za watu wa asili hususan Wamasaai inanuia kuwawezesha wanawake sio tu kiuchumi lakini pia kijamii. Basi kwa undani wa makala hii ungana na Grace Kaneiya.

Muziki waleta nuru kwa wakimbizi wa Syria nchini Ugiriki

Vita nchini Syria vimeingia mwaka wa 7 na mamia ya maelfu ya raia wamekimbia nchi hiyo kwani si shwari tena. Maisha ambayo wananchi walikuwa wamezoa yametumbukia nyongo. Hata hivyo hata kule walipo wanatafuta mbinu ya kuweza kuishi na kutumia stadi zao ili kukabiliana na machungu. Miongoni mwao ni mkimbizi kutoka Syria aliyeko Ugiriki ambaye anatumia ujuzi wake. Je anafanya nini? Ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Usaidizi wa kibinadamu ni muhimu sana hasa kwa wakimbizi

Wahenga walinena siri ya mtungi aijuaye kata, hawakukosea kwani madhila ya mtu anayejua ni amsaidiaye. Na hili limethibitishwa na Bi Khadija Hussein, afisa wa masuala ya ulinzi wa wakimbizi kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya. Baada ya kuhudumu hapo kwa miaka mingi. Leo Bi khadija amemweleza Flora Nducha wa Idhaa hii kwamba sasa anatambua ni kwa nini kazi wanayoifanya kama wahudumu wa kibinadamu ina umuhimu mkubwa kwa maisha ya wakimbizi na kwa kwao pia na ndio maana siku ya kimataifa ya utu wa kibinadamu itakayoadhimishwa Agosti 19 ina maana kubwa..

Vijana kushirikiana katika kufanikisha SDGs: Tanzania

Umoja wa Mataifa unapigia chepuo vijana kuwa bega kwa bega katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan lile la kwanza la kutokomeza umaskini bila kusahau usawa wa kijinsia. Na ni kwa mantiki hiyo shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UNWomen nchini Tanzania mwaka 2015 lilizindua programu ya maendeleo endelevu kupitia ujasiriamali, ikilenga vijana wa kike walio maeneo ya mipakani na nchi hiyo.

UN Photo/B Wolff

Mjadala kuhusu umuhimu wa unyonyeshaji watoto Burundi

Ulimwengu  umehitimisha wiki ya kunyonyesha juma hili, wataalamu wa shirika la afya ulimwenguni  (WHO) wakichagiza kuwa faida za kunyonyesha sio tu kwa watoto lakini kwa jamii nzima hasa katika swala nzima la uzazi wa mpango.

Ingawa kinamama wazazi wengi wanachangamkia utaratibu huu wa kunyonyesha watoto, baadhi ya wanawake wamejenga hoja nyingi za kutonyonyesha watoto.

Burundi ni miongoni mwa nchi ambazo, serikali imeshikia bango suala la unyonyeshaji hasa miezi sita ya mwanzo mtoto akizaliwa.

Mzazi ni mdau muhimu kuzuia mimba utotoni

Mzazi ni mdau muhimu katika kuzuia mimba za utotoni nchini uganda na kuhakikisha watoto wanatimiza ndoto za maisha hayo. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego leo amejikita katika changamoto hiyo ya mimba za utotoni na nini wajibu wa mzazi kuahikisha tatizo hilo linapunguzwa au kukomeshwa kabisa. Ungana naye katika makala hii kwa udani zaidi.

Mradi wa kutumia biogesi kupikia ni faraja kwa wakazi, Yatta Kenya

Matumizi ya biogesi iliotengenezwa kutokana na kinyesi cha wanyama na taka za nyumbani yanaboresha maisha hususan ya wanawake ambao hutumia hadi saa tatu kila siku kusaka kuni.

Mbinu hii inayojali mazingira na kuzuia kero itokanayo na matumizi ya kuni kupikia imeleta faraja kwa wakazi katika wilaya ya Yatta nchini Kenya. Kufahamu zaidi basi ungana na Grace Kaneiya katika makala ifuatayo.

Albino wamekosa nini hata wanyanyapaliwe na kuuawa?:Nyapinyapi

Watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino wamekosa nini hata wakatwe, viungo hata kuuwawa ? anahoji mwanamuziki wa Tanzania Azizi Kimindu Nyapinyapi katika kibao alichokitoa mahsusi kuelimisha jamii dhidi ya ukatili na mauaji ya watu hao.

Kufahamu zaidi kwa nini aliamua kutunga kibao hico na wito wake kwa jamii ungana na Flora Nducha na mwanamuziki huyo katika makala hii.