Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

(Picha:UN/Aliza Eliazarov)

Tumesikitishwa na kushtushwa na shambulio dhidhi ya walinda amani wetu:Mahiga

Tumeshtushwa sana na kusikitishwa na shambulio la jana dhidi ya walinda amani wetu. Amesema hayo waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga alipozungumza leo na Flora Nducha wa idhaa hii kufuatia kuuawa kwa walinda amani wa Tanzania 14, wengine 38 kujeruhiwa wakiwemo walio hali mahtuti na wanne kutojulikana walipo huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, baada ya kundi la waasi wa ADF kuzamia kituo cha walinda amani hao.

(MAHOJIANO KATI YA FLORA NDUCHA NA BALOZI AUGUSTINE MAHIGA)

Utokomezaji ukatili kwa wanawake sio jukumu la wanawake pekee bali jamii nzima: UM

Vita ya kupinga  ukatili dhidi ya wanawake katika mifumo yote ni moja vipaumbele katika  ajenda ya Umoja wa mataifa ya  maendeleo ya mwaka 2030.

Juma hili likiwa ni la maadhimisho ya siku yakutokomeza ukatili dhidi ya wanawake duniani itakayofikia kilele chake kesho  tarhe 25 Novemba ,  mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa pamoja na asasi za kiraia walijumuika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa new York Marekani kuunga mkono agenda vita hivyo.

Tanzania tunaelekea kulinda amani CAR na Sudan Kusini- Dkt. Mwinyi

Mkutano wa masuala ya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa umekunja huko Vancouver, Canada kwa lengo la kuangazia jinsi ya kuboresha operesheni hizo. Idadi kubwa ya operesheni ziko barani Afrika ambako mizozo na vita imegubika eneo hilo. Miongoni mwa washiriki alikuwa Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa kutoka Tanzania Dkt. Hussein Mwinyi. Kando mkutano huo Mathew Wells wa Idhaa ya Umoja wa Matafa alizungumza naye katika mahojiano haya ambayo maswali yataletwa kwako na Flora Nducha. Kwanza Dkt.

Kutoka Tanzania hadi Sudan Kusini kusaidia ulinzi wa raia- Meja Paschal

Maafisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania, JWTZ ni miongoni mwa watendaji katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani huko Sudan  Kusini, UNMISS. Maafisa hao wana majukumu mbalimbali yote yakichangia kufanikisha ulinzi wa raia na amani kwenye taifa hilo change zaidi duniani ambalo sasa limegubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwezi disemba mwaka 2013. Je ni yapi miongoni mwa majukumu hayo?

Hali ya mjane kutoka Uganda ni msumari wa moto juu ya kidonda-sehemu 1

Wakati Umoja wa Mataifa ukichagiza nchi kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma kuelekea ukomo wa malengo ya maendelo endelevu yaani SDGs bado kuna changamoto ambazo huenda zikakwamisha ufikiaji wa malengo hayo. Wanawake na waisichana mara kwa mara wanakabiliwa na aina mbali mbali ya ubaguzi ikiwemo suala la urithi wa mali hususan katika jamii zilizoko nchi zinazoendelea.

Ubunifu wa nguo za magome ya miti na uhifadhi wa mazingira Burundi-sehemu 1

Katika  Juhudi za kuunda ajira na  kuhifadhi mazingira, msichana kutoka Burundi Annick Kabatesi ameanzisha mradi wa kutengeneza nguo zitokanazo na magome ya miti.  Nguo hizo zimetajwa kuwa zinazingatia uhifadhi wa mazingira. Bi. Kabatesi ambaye ni mwanamitindo pia amejijengea umaarufu mkubwa kwa  kutengeneza nguo hizo za magome ya miti  baada ya nguo hizo kuwavutia viongozi wakuu Serikalini.

Tuangazie yanayotuweka pamoja badala ya migawanyiko- Ruteere

Katika zama za sasa, siasa zinaghubikwa na mwelekeo wa baadhi ya vyama kujipatia umaarufu kupitia ajenda za kibaguzi kutoka kwa wafuasi wao. Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya haki za binadamu imekuwa ikipaza sauti kupinga mwelekeo huo ukisema kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Hoja hiyo na nyingine nyingi ni miongoni mwa mambo ambayo Joseph Msami amezungumza na mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa zama za sasa Mutuma Ruteere ambaye amekamilisha jukumu lake tarehe 31 mwezi wa Oktoba mwaka huu wa 2017.

Vijana kushiriki kilimo si kosa- Restless Development sehemu 2

Vijana vijana vijana! Umoja wa Mataifa unasema ndio muarobaini wa kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Na ni kwa mantiki hiyo wakati wa mikutano ya ngazi ya juu ya mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, vijana kutoka pande mbalimbali za dunia walifika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuelezea kile wanachofanya mashinani ili kusongesha ajenda ya maendeleo na wakati huo huo kukwamua maisha yao.

Tanzania yaongeza vituo vya uchunguzi wa TB ili kufikia watu wengi zaidi

Hii leo shirika la afya ulimwenguni WHO limetoa ripoti kuhusu hali ya ugonjwa wa Kifua Kikuu au TB duniani ambapo kuna matumaini na wakati huo huo bado kuna changamoto. Mathalani WHO inasema idadi ya vifo kutokanana TB ilipungua kwa visa 400,000 ikilinganishwa mwaka jana na miaka 16 iliyopita. Na wakati huo huo kuna changamoto ikiwemo kuwafikia wagonjwa ambao wanakosekana katika kupima na kupatiwa tiba bara la Afrika ikiwa ni miongoni. Ni kwa mantiki hiyo Assumpta Massoi amezungumza na Dkt.