Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hedhi salama ni muarobaini katika kumuokoa msichana- Rebecca

Hedhi salama ni muarobaini katika kumuokoa msichana- Rebecca

Pakua

Vijana ndio tegemeo kubwa hivi sasa la Umoja wa Mataifa katika kusaka suluhu za changamoto zinazokumbwa ulimwengu. Ni kwa kutambua hilo chombo hicho chenye nchi wanachama 193 kinatumia uthabiti wa kundi hilo kuleta mabadiliko mashinani kwa kutambua uwezo wa vijana katika kuelewa na kuabdili maisha yao na ya wenzao. Kwa mantiki hiyo kando ya mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, viongozi vijana kutoka nchi mbali mbali walipata fursa ya kukutanishwa na viongozi walio madarakani hivi sasa ili kujadili mustakhbali wa dunia. Miongoni mwa vijana hao ni Rebecca Gyumi, muasisi na mwenyekiti wa Msichana Initiative, shirika linalohaha kufanikisha ndoto za mtoto wa kike na wasichana nchini Tanzania. Je nini amejifunza kwenye kikao hicho? Assumpta Massoi amezungumza naye ambapo pamoja na kufafanua umuhimu wa hedhi salama anaanza kwa kuelezea alichojifunza kwenye kikao chao na viongozi.

Photo Credit
Rebecca Gyumi, muasisi na mwenyekiti wa Msichana Initiative. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili