Tutaangalia mitaala yetu ili isaidia kukabili mabadiliko ya tabianchi- Balozi Mulamula
Mabadiliko ya tabianchi na athari zake kijamii ilikuwa ni moja ya mada wakati wa wiki ya Afrika iliyotamatishwa hivi karibuni kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Mathalani washiriki waliangazia siyo tu mabadiliko hayo yanavyoatishia amani na usalama bali pia mwenendo wa uhamaji hususan wakulima na wafugaji.