Haikuwa rahisi,wakimbizi wa Burundi waanza kurejea nyumbani: UNHCR
Pakua
Hatimaye kundi la kwanza la wakimbizi wa Burundi walioko nchini Tanzania limewasili nchini mwao, hii ni baada ya sintofahamu iliyosababisha mkutano kati ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, serikali ya Tanzania na Burundi.
Urejeshwaji wa wakimbizi hao kwa hiari umeanza kutekelezwa ambapo wakimbizi 300 wamewasili Burundi kurejelea maisha kwa kile kinachoaminika kuwa ni usalama kuimarika nchini mwao.
Kufahamu mchakato wa kuwarejesha wakimbizi na namna ulivyogubikwa na changanmoto kadhaa, Joseph Msami amezungumza na Mwakilishi Mkazi wa UNHCR nchini Burundi Abel Mbilinyi.