Tukihifadhi mazingira leo tunaepuka gharama kubwa Kesho
Pakua
Wana mradi wa kuruwitu kutoka Kilifi Mombasa nchini Kenya, wametoa wito wa kuhifadhi mazingira leo ili kuepuka athari zake katika kizazi kijacho. Shida Magunda na Katana Ngala Hinzano wako katika mradi wa kuhifadhi mazingira ya bahari Mombasa kwa kutumia uzalishaji wa samaki. Mradi wao ambao ni wa kwanza nchini Kenya pi umetunukiwa tuzo ya mazingira ya Equator inayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na Equator initiative. Wamezungumza na Flora Nducha na Katana Ngala anaanza kueleza historia ya mradi