Ukame waathiri usafiri wa majini kupitia Ziwa Albert Uganda
Pakua
Mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri katika masuala mbalimbali ikiwemo huko nchini Uganda ambako mwaka huu nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa nchi ambazo zimekabiliwa na ukame wa muda mrefu.
Kando na kusababisha njaa katika nchi za Afrika Mashariki pia moja ya athari ni kupungua kwa kiwango cha maji katika Ziwa Albert tangu Machi kulikokwamisha usafiri wa majini.Basi ungana na John Kibego katika makala hii inayokupa taswira ya hali ilivyo kwa sasa.