Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

06 OKTOBA 2021

Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea

-Janga la utapiamlo limefurutu ada nchini Afghanistan , huku mabadiliko ya tabianchi na vita vinadhidisha madhila kwa watoto na familia zao yameonya mashirika ya Umoja wa Mataifa la UNICEF na WFP

-Mradi wa uvuvi wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO ujulikanao FISH4ACP baada ya kushamiri Kigoma Tanzania sasa umehamia mkoani Katavi kuwaletea nuru wavuvi

Sauti
14'24"

05 OKTOBA 2021

Katika Jarida la Habari ya Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea 

-Janga la COVID-19 limewaathiri watoto kwa kiasi kikubwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema ni mwiba kwa afya ya akili kwa vijana na watoto

-Leo ni siku ya waalimu duniani UNESCO na wadau wanazihimiza serikali kuwapa waalimu kipaumbele katika kurejesha elimu mahali pake na kurejesha matumaini ya watoto wengi.

Sauti
14'5"

04 OKTOBA 2021

Katika Jarida la Habari hii leo  kutoka Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres akifungua mkutano wa 15 wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendfeleo na biashara UNCTAD15 mjini Bridgetown Barbados ametoa wito wa kuhakikisha usawa wa biashara, uwekezaji na na kujikwamua vyema na COVID-19

-Ripoti ya kamati huru ya uchunguzi wa haki za binadamu nchini Libya imesema kuna ushahidi kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaoweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ulitekelewa nchini humo tangu 2016

Sauti
15'10"

Jarida Octoba 1 2021

Ni ijumaa ya tarehe Mosi mwezi Octoba mwaka 2021 karibu uungane na Assumpta Massoi kusikiliza jarida ambapo kama ilivyo ada ya kila Ijumaa tunakuletea mada kwa kina, leo tutakuleta mahojiano na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Peter Mathuki alipohudhuria mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA76, jijini New York Marekani.

Sauti
12'25"

Jarida 30 Septemba 2021

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya sekta ya bahari , janga la corona au COVID-19 limethibitisha umuhimu wa bahari na kujitolea kwa mamilioni ya mabaharia wanaofanyakazi katika sekta hiyo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Karibu usikilize jarida linaloletwa kwako na Assumpta Massoi ambapo atakujuza kwa undani taarifa hiyo na nyingine nyingi.

Sauti
12'14"

Jarida 29 Septemba 2021

Karibu usikilize jarida ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha kuhusu upotevu na utupaji wa chakula na mwenyeji wako ni mimi ASSUMPTA MASSOI. 

Miongoni mwa utakayo sikia ni pamoja na programu ya UNICEF nchini Kenya yawasaidia watoto wa kike kurejea shuleni. 

Taasisi ya kusaidia wakimbizi wandani nchini Yemen yashinda Tuzo ya UNHCR ijulikanayo kama tuzo ya wakimbizi ya Nansen. 

Audio Duration
14'2"

Jarida 28 Septemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo utasikia shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO na wadau wake wamezindua mkakati wa kwanza wa aina yake wa kutokomeza ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo, ugonjwa ambao unaua mamia ya maelfu ya watu kila mwaka.

pia utasikia taarifa nyingine kuhusiana na nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia Kongo - DRC 

Sauti
13'46"

Jarida 27 Septemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo utasikia sehemu ya pili ya mahojiano yaliyofanywa na Anold Kayanda na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. 

Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangalizia siku ya utalii duniani ambayo huadhimishwa leo Septemba 27.

Sauti
12'40"

Jarida 24 Septemba 2021

Ni Ijumaa ya tarehe 24 mwezi Septemba mwaka 2021 karibu kusikiliza jarida na kama ilivyo ada ya kila Ijumaa tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakuletea sehemu ndogo ya mahojiano marefu na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania baada ya hapo jana kuhutubia kwa mara yake ya kwanza katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Sauti
12'6"

Jarida 23 Septemba 2021

Ni Alhamisi  ya tarehe 23  ya mwezi Septemba mwaka 2021 siku ya tatu ya mjadala mkuu wa mikutano ya ngazi ya juu ya Umoja wa Mataifa

Miongoni utakayo sikia kwenye jarida hii leo ni pamojana Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassana ahutubia mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa, UNGA76 akizungumziamasuala kadhaa ikiwemo ushirikiano wa kimataifa na ahadi yake kwa jumuiya ya kimataifa. Halikadhalika tunakwenda Ethiopia na pia Cameroon. Makala ni Uganda na mashinani tunakutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Sauti
9'56"