Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

31 Machi 2021

Hali ni tete Cabo Delgado, mashirika ya UN yahaha kunususu raia. Huduma kwa wajawazito Libya zinazowezeshwa na UNHCR mkombozi wa wakimbizi wa Eritrea. Nchini Kenya kampeni ya kulinda wanyamapori nayoongozwa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP imezidi kupanua wigo wake ambapo hivi sasa hata watu ambao awali walikuwa adui wa wanyamapori, wamegeuka rafiki na walinzi wakuu wa wanyama hao kama njia mojawapo ya kuhifadhi misitu kama ile ya mlima  Kenya.

Sauti
12'7"

30 Machi 2021

UNICEF yawezesha mtoto mkimbizi kuwa na ndoto ya kuwa daktari.  Msaada wa IFAD umeniokoa mimi na familia yangu, asema Mjasiriamali Fatou Secan wa Gambia. Na mkimbizi kutoka Syria aeleza namna Ovale Citoyen ya Ufaransa wamemrudisha michezoni. 

Sauti
11'43"

29 Machi 2021

Kikosi cha 13, TANZBATT-13, cha wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani jimboni Darfur nchini Sudan kupitia UNAMID ambao ni ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Africa, AU, kimetamatisha jukumu lao na leo tunamulika tathmini yao wenyewe kama anavyosimulia Koplo Japhet Chakula, afisa habari wa TANZBATT-13.

Sauti
10'10"

26 MACHI 2021

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea

-Umoja wa Mataifa leo unapeperusha bendera zake katika Makao Makuu na mkatika ofisi zake kote duniani nusu mlingoti ili kumuenzi  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli aliyefariki dunia 17 Machi na kuzikwa leo Chato mkoani Geita Tanzania

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limefanikiwa kuwafikia wakimbizi kKaskazini mwa jimbo la Tigray Ethiopia kwa mara ya kwanza tangu Novemba mwaka jana 2020

Sauti
15'54"

25 MACHI 2021

Katika Jarida la Habari za UN hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR laisihi serikali ya Kenya kuhakikisha maamuzi kuhusu kufunga kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab yanaheshimu haki za wakimbizi na kuwa ni suluhuhisho muafaka na endelevu

-Katika siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa katika bahari ya atlantiki Katibu Mkuu Antonio Guterres anataka kuwaenzi waathirika wa utumwa na biahsra hiyo kwa kuanika bayana historia na madhila waliyopitia na kuhakikisha yanakomeshwa

Sauti
13'5"

24 MACHI 2021

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea 

- Ikiwa leo ni siku ya kifua Kikuu duniani Umoja wa Mataifa umetangaza habarin njema ya tiba ambayo sio tu gharama yake ni nafuu bali pia ni ya muda mfupi na vidonge vinavyotumika ni vichache.

-Mashirika ya Umoja wa Mastaifa yaendelea kufikisha nuru kwa wakimbizi huko Ituri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwa misaada mbalimbali ya kibinadamu

Sauti
12'37"

23 MACHI 2021

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Watu 670,000 wamelazimika kuzikimbia nyumba zao hadi sasa huko Cabo Delgado Msumbiji kufuatia kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya raia limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

- Leo ni siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema maji na hali ya hewa ni lila na fila havitengamani

Sauti
13'54"

22 MACHI 2021

Katika jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Grace Kaneiya anakuletea

-Leo ni siku ya maji duniani na Umoja wa Mataifa umesisitiza kila mtu kutambua thamani ya rasilimali hiyo muhimu ili kuhakikisha watu wote wana fursa ya kuipata kote duniani

-Nchini Sudan Kusini mpango wa Umoja wa Mastaifa UNMISS umeendesha warsha ya siku mbili Yambio na Nzara kwa ushirikiano na serikali ili kuhakikisha vijana, wanawake na jamii wanajikwamua vyema na janga la COVID-19, vita na mabadiliko ya tabianchi

Sauti
12'33"

18 MACHI 2021

Katika Jarida maalum la Umoja wa Mataifa hii leo, Grace Kaneiya anakuletea

-Salamu za rambirambi  zaendelea kutolewa kutoka Umoja wa Mataifa, mashirika yake na viongozi mbalimbali kufuatia kifo cha Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kilichotokea jana Machi 17

- Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Profesa Kennedy Gastorn amesema Tanzania, Afrika na jumuiya ya kimataifa imepoteza kiongozi mwenye uthubutu na daima ataenziwa John Magufuli

-Wananchi wa Tanzania wamuomboleza Rais wao aliyeaga dunia jana Machi 17

Sauti
12'38"

17 Machi 2021

COVID-19 kuingilia huduma za afya kumechangia vifo 239,000 vya kina mama na watoto Asia Kusini:UN 

UNHCR na wadau wa misaada wazindua ombi la dola bilioni 1.2 kusaidi wakimbizi wa Sudan Kusini

Hali ya wanawake ni hali ya demokrasia – Kamala Harris 

Makala imejikita nchini Tanzania na mashinani ni kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA

Sauti
12'45"