Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

05 OKTOBA 2021

05 OKTOBA 2021

Pakua

Katika Jarida la Habari ya Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea 

-Janga la COVID-19 limewaathiri watoto kwa kiasi kikubwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema ni mwiba kwa afya ya akili kwa vijana na watoto

-Leo ni siku ya waalimu duniani UNESCO na wadau wanazihimiza serikali kuwapa waalimu kipaumbele katika kurejesha elimu mahali pake na kurejesha matumaini ya watoto wengi.

-Nchini Sudan Kusini ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kutegua mabomu ya kutegwa ardhini UNMAS inasema mabomu hayo ni hatari kubwa kwa jamii na inaendelea na hatua za kuyasafisha yote

-Makala yetu leo inatupeleka Tanzania kwa bondia wa kike ambaye anataka kujenga shule ya kuinua vipaji wa bondia kwa wanawake.

_Na mashinani tunabisha hodi Kenya kuangalia umuhimu wa kuboresha mifumo ya chakula kwa ajili ya lishe ya watoto

Audio Credit
UN News/Assumpta Massoi
Audio Duration
14'5"