Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

Jarida 31 Agosti 2021

Katika Jarida hii leo Grace Kaneiya atakujuza kuhusu vyeti vya Covid-19 kwa njia ya kielektroniki. 

Pia utasikia namna matumizi ya tehama yalivyowasaidia wanafunzi nchini Kenya kuongeza ufaulu na kupunguza utoro na huko Bangladesh wakulima wanafurahia uwekezaji wa FAO. 

Karibu usikilize kwa undani. 

Sauti
13'51"

Jarida 30 Agosti 2021

Katika jarida hii leo tutamsikia kwa kirefu Mhandisi Dkt.Alinda Mashiku, mwanamke Mtanzania anaye ng'ara katika kituo cha safari za anga cha Marekani NASA  tawi la Goddard mjini Maryland lililojikita na ufuatiliaji wa safari za satellite.

Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia misaada nchini Afghanistan. 
 

Jarida 27 Agosti 2021

Katika Jarida hii leo utasikia wavuvi kutoka Kigoma nchini Tanzania wanavyojikinga na janga la Corona au COVID-19  pamoja na kile wasemacho juu ya  chanjo ya ugonjwa huo.

Pia utasikia habari kutoka maeneo mbalimbali lakini kubwa ni milipuko iliyotokea karibu na uwanja wa ndege wa Kabul nchini Afghanistan tarehe 16 Agosti 2021.

Sauti
12'50"

Agosti 26 2021

Katika jarida hii leo Grace Kaneiya anakuletea taarifa kutoka Afghanistan ambapo WFP inaeleza kukabiliwa na uhaba wa chakula. 

Pia utasikia UNMISS wanavyoenesha doria Sudan Kusini, na mkimbizi wa Ethiopia aliyepata fursa ya kwenda masomoni nchini Italia. 

Sauti
12'33"

Agosti 25, 2021

Katika jarida hii leo utamsikia Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni Tedros Ghebreyesus akizungumzia udhalimu wa usambazaji chanjo Afrika na nini kifanyike.

Pia utasikia mengi ikiwemo wakimbizi kutoka Afghanistan wamewasili nchini Uganda 

Sauti
11'58"

Jarida 24 Agosti 2021

Hii leo katika jarida utasikia kuanza kwa mashindano ya kimataifa ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu mjini Tokyo Japani yakihusisha washiriki wa michezo mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wakiwemo wakimbizi. 
Pia utasikia kutoka Geneva Uswisi Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu ambalo limetuma ujumbe kwa Taliban nchini Afghanistan

Sauti
13'45"

23 Agosti 2021

Tuliyokuandalia hii leo kutoka Umoja wa Mataifa:

Tuna habari muhimu za siku na katika mada yetu kwa kina tutaelekea nchini Kenya kukutana na manusura wa shambulio la bomu la Kenya la mwaka 1998.

Na Katika mashinani, leo tutaelekea nchini Tanzania kusikia kuhusu midahalo inayoandaliwa na asasi ya vijana wa Umoja wa Mataifa.
 

Sauti
12'17"

Jarida 20 Agosti 2021

Hii leo katika jarida utasikia mahojiano na manusura wa Covid-19, Bwana Ole Pertet, mmoja wa wakazi wa Marekani waliougua mwanzoni kabisa ugonjwa huo ulipoingia Marekani. 

Lakini kabla ya mada hiyo utasikia habari kwa ufupi ambapo kuelekea siku ya kimataifa ya kumbukumbu na kuwaenzi waathirika wa ugaidi, itakayoadhimishwa hapo kesho Agost 21, leo kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa ngazi ya juu kuwaenzi waathirika hao ukijikita  zaidi katika msaada wa kisaikolojia na ulinzi kwa waathirika.  

Sauti
11'16"

Jarida 19 Agosti 2021

Leo ni siku ya wahudumu wa masuala ya kibinadamu duniani ambao wako msitari wa mbele kusaidia kuokoa maisha ya watu walio hatarini zaidi duniani majanga yanapozuka, na kwa kufanya hivyo huweka rehani maisha yao kila uchao amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifaifa Antonio Guterres

Je umewahi kujiuliza ni kwa nini wakati mwingine misaada ya kibinadamu husambazwa kwa njia ya gharama zaidi ya ndege kudondosha misaada hiyo kutoka angani? 

Na Umoja wa Mataifa umetoa milioni 8 kusaidia nchi ya Haiti 

Sauti
11'46"

Jarida 18 Agosti 2021

Katika jarida hii leo utasikia kuhusu uzinduzi wa mkakati wa Mabadiliko ya Kidigitali ya Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa. Pia utasikia wakimbizi wa ndani nchini Somalia wanavyoteseka na njaa pamoja na utoaji chanjo kwa wakimbizi wa Rohingya huko kambini Coxs Bazar.

katika makala leo tunaangazia utunzaji wa mazingira kwa vijana nchini Rwanda. 

Sauti
13'7"