Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

30 Julai 2021

Jaridani na Assumpta Massoi-

Leo ikiwa ni Ijumaa ni mada kwa kina ambapo tunaendeleza makala ya homa ya ini, pia kuna habari kwa ufupi zikiangazia habari muhimu ya siku. Katika neno la wiki inachambuliwa methali Atangaye na jua hujua!

Sauti
10'43"

Julai 29, 2021

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umepatia mafunzo ya mbinu za medani 

Nchi ya Bhutan yafanikiwa kutoa chanjo kwa 90% ya watu wake wanaotakiwa kupata chanjo

Pia utasikia makala ya binti mdogo manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu aliyesafirisha bila ridhaa yake na kubakwa.

Sauti
12'23"

28 Julai 2021

Jaridani Jumatano 28, 2021 

Hii leo huko nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kazi ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19.

Uwekezaji wa kupambana na ugonjwa wa homa ya ini wazaa matunda.

Mkataba wa wakimbizi watimiza miaka 70 leo.

Sauti
13'41"

27 Julai 2021

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia Roma nchini Italia kunakofanyika mkutano tangulizi wa viongozi kuhusu mifumo ya chakula duniani, kisha anakwenda Sudan Kusini ambako huko walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Thailand wanatekeleza kauli ya wahenga kuwa mfundishe mtu kuvua samaki badala ya kumpa samaki mmoja. Anasalia huko huko Sudan Kusini akimulika adha ya wakimbizi wa ndani waliofurushwa Tambura jimboni Equatoria Magharibi. Makala ni kuhusu wakimbizi wa ndani nchini Uganda na wito wao kwa serikali kuwapatia eneo la kuishi.

Sauti
13'24"

26 Julai 2021

Jaridani Julai 26, 2021 na Assumpta Massoi

Jaridani ni habari kwa ufupi na makala ya kina ikiangazia homa ya ini kuelekea siku ya homa ya ini ambayo huadhimishwa kila mwaka Julai 28. Na katika mashinani tutakuwa nchini Tanzania.

Sauti
11'34"

23 Julai 2021

Jaridani Ijumaa Julai 23, 2021-

Ikiwa leo ni Ijumaa tuna habari kwa ufupi na mada kwa kina ambayo ni simulizi ya muuguzi aliyepata COVID-19 na kisha kupona pia neno la wiki ambapo mchambuzi wetu anachambua neno "basi"

Sauti
12'19"

22 Julai 2021

Jaridani Julai 22, 2021 tunaangazia-

Wakulima Ethiopia waeleza namna wanavyotaka changamoto za kilimo zitatuliwe.

Hali ya chanjo nchini Malawi baada ya UNICEF kuingilia kati.

Wafungwa nchini CAR wapata stadi za maisha baada ya kifungo.

Mashinani tutaelekea kambini nchini Lebanon.

 

Sauti
11'37"

21 Julai 2021

Jaridani Julai 21, 2021-

UN yaendelea kuwasaidia wakimbizi wa ndani walioyakimbia mashambulizi katika makazi yao Sudan Kusini.

UNHCR yawajengea makazi wakimbizi wa ndani DRC.

Mradi wa Benki ya Dunia Ghana waleta furaha kwa kaya maskini.

Sauti
11'49"

19 Julai 2021

Jaridani Julai 19, 2021-

Jarida limeanza na mukhtasari wa habari muhimu, makala yetu la leo inaangazia ujumuishwaji wa vijana katika kufanikisha mfumo endelevu wa chakula kuanzia shambani hadi mezani. Na mashinani ni mafunzo kwa wakulima huko Jordan kwa ufadhili wa shirika la kazi duniani. ILO.

Sauti
10'24"

16 Julai 2021

Jaridani Ijumaa Julai 16, 2021 na Assumpta Massoi-

Mada kwa kina leo inaangazia ufugaji kuku nchini Uganda na katika neno la wiki tunasikia ufafanuzi wa neno mauja kutoka BAKITA.

Sauti
10'1"