Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

31 DESEMBA 2021

Katika jarida la matukio ya mwaka la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Wanajeshi watatu wa kulinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, wamejeruhiwa na mmoja vibaya sana baada ya msafara wao kukanyaga vilipuzi. Wote wanatibiwa hospitalini mjini Bangui

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema mwaka huu umekuwa wa machungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto katika mizozo ya muda mrefu na ile mipya. 

Sauti
12'7"

30 DESEMBA 2021

Katika Jarida la habari hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Kenya limechukua hatua ya kushirikiana na viongozi wa dini ikiwemo wale wa madhehebu ya kiislamu ili kusaidia kuelimisha waumini wao juu ya chanjo ya COVID-19 na faida zake katika kuepusha maambukizi

-Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na masuala ya afya ya uzani UNFPA limezindua kampeni ya Hakimiliki ya mwili kwa lengo la kukabiliana na ukatili wa kijinsia mtandaoni hususan dhidi ya wanawake na wasichana 

Sauti
12'6"

29 Desemba 2021

Hii leo jaridani ni siku ya nada kwa kina tukibisha hodi kwenye makazi ya wakimbizi ya Kyangwali huko Hoima nchini Uganda kusikia tathmini ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuhusu mwaka huu wa 2021 na matarajio yao kwa mwaka 2022. Hata hivyo kuna habari kwa ufupi ikiwa na salamu za mwaka mpya za Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitaka dunia iazimie kuwa mwaka 2022 ni mwaka wa kujikwamua kutoka kwenye madhila. Na mashinani tunabisha hodi Ufilipino, taifa lililopigwa na kimbunga Rai mwezi huu na sasa wananchi wanaelezea kile walichoshuhudia.

Sauti
11'10"

28 Desemba 2021

Hii leo jarindani tunaanzia nchini Cote D’Ivoire ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeleta matumaini makubwa kwa wakimbizi ambao maisha yao kiuchumi yalitwamishwa na COVID-19. Kisha tunasikia ujumbe wa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kuhusu mwelekeo wao wa 2022 na mafanikio yao mwaka 2021 hasa kutokana na kujumuisha vijana katika kufanikisha upatikanaji wa chakula. Tunabisha hodi pia Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako walinda amani wa Tanzania #TANBAT5 wanatuma salamu za mwisho wa mwaka na heri ya mwaka mpya huku wakitoa shukrani.

Sauti
12'46"

27 Desemba 2021

Hii leo jaridani ni mada kwa kina na leo tunabisha hodi nchini Tanzania kuangazia harakati za Umoja wa Mataifa kupitisha shirika lake la chakula na kilimo, FAO za kusongesha kilimo hifadhi kama njia mojawapo ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDG sambamba na kukabiliana na madhara ya tabianchi. Tunapata pia  kwa ufupi habari zilizopatiwa kipaumbele siku ya leo bila kusahau mashinani ambapo tunabisha hodi nchini  Kenya kwa wazee wa jamii ya kiduruma wakijakuelimisha jinsi wanavyohesabu miezi kwa lugha ya kiduruma badala ya kutumia Januari, Februari na kadhalika.

Sauti
11'35"

23 Desemba 2021

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia nchini Burundi ambako kijana mmoja baada ya kumaliza masomo ya elimu ya juu na kuona cheti chake hakimpatii ajira aliamua kuanzisha mradi wa kuku na sasa amekuwa chachu kwa jamii yake! Huko Tanzania watoto wamuandikia barua Rais Samia Suluhu Hassan kulikoni? Na kisha ni nchini Mali ambako tofauti za tamaduni zatumika kujenga amani badala ya mvuragano. Makala tunabisha hodi nchini Uganda na mashinani tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kusikiliza faida za rumba!!! Karibu!

Sauti
14'9"

22 Desemba 2021

Hii leo jaridani ni mahsusi kabisa kwa kukutakia sikukuu njema ya Krismasi na mwaka mpya 2022 wenye ustawi na salamu ni kutoka kwa wanaidhaa ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa wengine walioko mashinani wadau wetu. Lakini pia kuna habari kwa ufupi kuhusu Yemen na mgao wa chakula, hali mbaya ya watoto Afghanistan bila kusahamu mashinani ujumbe mahsusi kutoka WHO wa kutaka watu wawe makini msimu huu wa sikukuu ili kuepusha maambukizi ya COVID-19. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Sauti
9'57"

21 Desemba 2021

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanza na kufurushwa kwa raia huko Cameroon hususan kutokana na ghasia eneo la kusini-mashariki. Kisha anakwenda Zambia ambako wakimbizi kutoka DRC wameamua kurejea nyumbani kwa hiari kutokana na hali ya usalama kuwa shwari. Na nchini Yemen katikati ya zahma na mizozo familia moja imepata faraha baada ya watoto wao mapacha waliokuwa wameungana kuanzia kifuani hadi tumboni kutenganishwa. Makala tunakwenda Kenya kumulika mpishi wa vyakula vya kiasili aliyepata umaarufu jijini Nairobi na hivyo kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs ya afya na ustawi.

Sauti
13'38"

20 Desemba 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anakuunganisha na Jason Nyakundi mwandishi wa habari wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya ambaye amezungumza na mwanamke aliyevunja mwiko wa uchaguzi wa kazi na kuamua kujitosa katika sekta ya ujenzi. Mashinani mashinani leo tunabisha hodi kwa Rais wa Baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswisi, na bila kusahau leo kwa kuwa ni mada kwa kina tunakuwa na habari kwa ufupi ikimulika ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa huko Lebanon, sambamba na vikao vya Baraza la Usalama vikiangazia hali ya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Audio Duration
10'30"

17 Desemba 2021

Karibu kusikiliza jarida, kama ilivyoada ijumaa tunakuleta mada kwa kina na hii leo ni kutoka katika taifa changa zaidi Afrika, Sudan Kusini huko tutasikia namna msanii wa uchoraji anavyoinua jamii yake hususan wanawake. 

pia utapata fursa ya kusikiliza habari kwa ufupi na kujifunza kiswahili 

Sauti
11'50"