Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

29 Januari 2021

Hii leo Ijumaa ni mada kwa kina , leo tutaelekea Nairobi, mji mkuu wa Kenya ambapo tutakutana na mfanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Wanja Munaita akielezea jinsi alivyoweza kutimiza ndoto yake kuanzia kusaidiwa na shirika hilo hadi yeye kusaidia wengine kupitia shirika hilo. Kuna habari kwa ufupi tukimulika ghasia Darfur, Sudan halikadhalika CAR na pia neno la wiki leo ni maana ya Ugua Pole! Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Sauti
10'45"

28 Januari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanza na vipaumbele vya mwaka huu wa 2021 vya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambavyo ni 10. Kisha anakwenda Tanzania kutamatisha sehemu ya pili ya taarifa kuhusu jinsi mashirika ya Umoja wa Mataifa yameleta kujiamini kwa wasichana Angel na Fatma. Kisha anabisha hodi huko Mediteranea ambako twaelezwa kuwa janga la tabianchi ukanda wa Sahel na ghasia pembe ya Afrika vyazidi kusukuma watu kusaka mbinu zote kuvuka baharí na kwenda Ulaya. Makala tunamaliza sehemu ya pili kutoka kwa Mzee Peter Semiga wa Uganda na pia kuna mashinani. Karibu!

Sauti
14'3"

27 Januari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanzia nchini Tanzania kumulika harakati za watoto wa kike na elimu, kisha anakukutanisha na wajasiriamali vijana kupitia shirika la maendeleo ya viwanda la Umoja wa Mataifa, UNIDO. Baada ya hapo anakupeleka Vietnam ambako utaalamu umemaliza tabia ya wakulima kuonja maji ili kutambua iwapo yana chumvi nyingi au la kabla ya kumwagilia kwenye mpunga. Makala tunakwenda Nairobi nchini Kenya ambako kijana aliyekuwa sugu mtaani sasa amegeuka mkombozi kwa vijana wengine waliokuwa tishio mitaani na anatamatisha na mashinani kutoka Sudan Kusini, karibu!

Sauti
13'43"

26 Januari 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anaanzia Msumbiji ambako kimbunga Eloise kimetonesha kidonda cha manusura wa vimbunga Chalane na Idai. Kisha atabisha hodi Burkina Faso akimulika raia waliokimbia vurugu makwao wakikumbwa na janga la mabadiliko ya tabianchi. Anabisha hodi pia Somalia ambako mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea jimbo la Galmudug. Makala tunakwenda kaunti ya Nakuru nchini Kenya kukukutanisha na Bibi Afya na mashinani tunasalia huko huko kusikia jinsi skauti wa Kenya wameamka sasa wanalinda mazingira. Karibu! 

Sauti
13'6"

25 Januari 2021

Hii leo mwenyeji wako Grace Kaneiya akiwa Nairobi Kenya anajikita katika mada kwa kina kutoka Zambia ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasaidia jimbo la Luapula kuwa na huduma za maji safi na kujisafi. Mashinani anasalia huko huko Kenya na mtoto akizungumzia masomo yalivyorejea sasa baada ya shule kufungwa kutokana na COVID-19 lakini pia kuna habari kwa ufupi. Karibu!

Sauti
10'27"

22 Januari 2021

Leo Ijumaa ni mada kwa kina ikijikita katika harakati za  ukuzaji wa lugha ya kiswahili nchini Tanzania na nje ya mipaka hiyo kupitia kufundisha lugha hiyo adhimu wageni bila kusahau umuhimu wa kujumuisha watu wenye ulemavu katika harakati hizo. Hata hivyo tuna Habari kwa Ufupi ikimulika ukanda wa Sahel, Sudan na Syria na mwishoni ni maana ya sentensi na mchambuzi ni Aida Mutenyo kutoka Uganda. Mwenyeji wako leo ni Grace Kaneiya.

Sauti
9'56"

21 Januari 2021

Jaridani hii leo tunaanzia na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa inayotia hofu kuwa penginepo wazee wakimbizi watakuwa hatarini zaidi barani Afrika kutokana na kuibuka tena kwa COVID-19, kisha tunakwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ambako machafuko mapya yameendelea kuwa changamoto kwa walinda amani na kumefanyika tukio maalum la kuwaaga walinda amani waliouawa. Baada ya hapo tunabisha hodi huko kaunti ya Nyeri nchini Kenya kuona jinsi vijana wamebadili ndizi kuwa utajiri wao!

Sauti
12'13"

20 Januari 2021

Habari njema! Idhaa yetu ya Kiswahili ya Umoja wa Maitafa yaibuka kidedea katika tuzo za kimataifa za Kiswahili za Shaaban Robert katika  ukuzaji wa msamiati! Hiyo ni habari kuu leo hii tukimulika pia wanadiplomasia na matumizi ya lugha hiyo adhimu kwenye Umoja wa Mataifa na maoni ya wachapishaji katika tamasha la Kiswahili nchini Tanzania. Tunamulika pia Cabo Delgado hali inazidi kuwa mbaya, na makala leo wananchi wa Uganda na maoni yao baada ya intaneti kurejeshwa. Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Sauti
11'42"

19 Januari 2021

Leo Jumanne tunamulika utoaji wa chanjo ya COVID-19 kwa wakimbizi huko Jordan, kisha tunakwenda Cameroon kumulika wakimbizi waliofurushwa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kutokana na machafuko nchini mwao. Huko Brazil tunamulika jinsi miti inatumika kufuta machozi ya familia zilizopoteza jamaa zao kutokana na COVID-19.

Sauti
12'29"

18 Januari 2021

Hii leo Jumatatu ni mada kwa kina tunapiga kambi Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO wanafundisha wakazi masuala ya TEHAMA, yaani teknolojia ya habari na mawasiliano. Mwenyeji wetu ni Luteni Issa Mwakalambo. Tuna pia  Habari kwa Ufupi tukimulika COVID-19, Darfur Sudan na Uganda. Mashinani tunakwenda Rwanda. Karibu msomaji wako leo ni Flora Nducha.

Sauti
11'54"