Juni 30 2021
Katika Jarida hii leo utasikia huko Paris nchini Ufaransa kumeanza jukwaa la siku tatu la kusaka kusongesha usawa wa kijinsia kwa kujumuisha vijana katika kufanikisha lengo hilo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa. Mkutano huo unafanyika kwa kuzingatia kuwa miaka 25 baada ya mkutano wa kimataifa wa wanawake huko Beijing nchini China, bado usawa wa jinsia unasalia ndoto kwa maeneo mengi.