Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

29 Oktoba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo kama ilivyo ada ijumaa tunakuletea mada kwa kina leo tukimulika usanifu majengo na udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi mijini kuelekea siku ya miji duniani tarehe 31 mwezi huu wa Oktoba.

Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia wito uliotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa duniani na mashirika mengine ya kimataifa tisa kuhusu maji na mabadiliko ya tabianchi. Taarrifa nyingine ni Maendeleo ya teknolojia kwa wanahabari na asasi za kiraia pamoja na mbinu bora na za kimkakati za kuwalinda watoto walioathiriwa na migogoro

Sauti
17'41"

28 Oktoba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo ASSUMPTA MASSOI anakuletea taarifa zikiwemo

-Mkutano unaohusu utafiti, sayansi teknolojia na uvumbuzi katika kukuza ushirikiano na maendeleo katika nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni sehemu ya mbio za kuyafikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs, ulioandaliwa na Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ya Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu umehitimishwa leo jijini Bunjumbura kwa kunuia kuwapa nafasi watafiti katika kukuza uchumi.

-Mradi wa chakula shuleni nchini Rwanda unatekelezwa na WFP. 

Sauti
12'6"

27 Oktoba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo tunakuletea mada kwa kina maalum kutokea Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC ikimulika michezo hususan mpira wa miguu na ulinzi wa amani ambako kumefanyika  mechi ya kirafiki kati ya Timu ya walinda amani kutoka Tanzania na wenyeji Lion Mavivi.

Pia utapata fursa ya kusikiliza habari kwa kifupi zikiangazia makubaliano ya kusambazwa dawa ya vidonge vya kutibu COVID-19 kwa wagonjwa wasio mahututi, utasikia pia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa Mataifa mashinani nchini Tanzania.

Sauti
11'38"

26 Oktoba 2021

Karibu usikilize jarida ambapo leo Assumpta Massoi amekuandalia habari mbalimbali zikiwemo

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP imeeleza kuwa ahadi mpya na zilizorekebishwa kuhusu viwango vya nchi vya kukabili mabadiliko ya tabianchi, NDCs hazijafikia lengo lililowekwa katika mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi na hivyo ulimwenguni kuwa hatarini kuwa na ongezeko la joto la angalau nyuzijoto angalau 2.7 katika karne hii.

Sauti
11'59"

25 Oktoba 2021

Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo katika mada kwa kina tutazungumzia mafunzo ya upishi wa chakula cha asili kwa watoto wakike na wakiume

Katika taarifa yetu ya Habari kwa ufupi tunaangazia mapinduzi ya kijeshi nchini Sudan na kauli zilizotolewa na viongozi wa Umoja wa Mataifa.

Sauti
11'37"

22 Oktoba 2021

Leo kama ilivyo ada ya Ijumaa tunakuletea mada kwa kina tukimulika siku ya Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa tarehe 24 mwezi huu wa Oktoba.

Pia tutakuletea taarifa ya Habari ambapo utasikia kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania kimeshambuliwa huko DRC na ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres kwa ulimwengu katika kuadimisha siku ya Umoja wa Mataifa.

Kipengele cha kujifunza kiswahili hii leo ni kutoka kwa mchambuzi kutoka Kenya akifafanua maana ya methali, "Ulivyoligema utalinywa" msemo "

Sauti
14'4"

21 Oktoba 2021

Karibu kusikilizia jarida ambapo miongoni na taarifa utakazo sikia hii leo ni pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu wanawake, amani na usalama ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati umefika kwa baraza hilo kuonesha kwa vitendo uungaji wake mkono wa harakati za wanawake katika ujenzi na uendelezaji wa amani badala ya kusalia maneno matupu. 

Sauti
13'36"

20 Oktoba 2021

Karibu uungane na Assumpta Massoi akikuletea mada kwa kina mahsusi ikimulika harakati za Umoja wa Mataifa za kuimarisha afya na kuinua kipato mashinani. 

Pia utapata fursa ya kusikia habari kwa ufupi zikieleza kuuawa kwa watoto nchini Syria katika Shambulio, msaada wa kibinadamu kwa nchi ya Madagascar na mkutano wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa unaoongozwa na Kenya. 

 

Sauti
9'54"

19 Oktoba 2021

Hii leo ASSUMPTA MASSOI  anakujuza mengi ikiwemo, watu mashuhuri 34 wanapanda mlima Kilimanjaro ili kuchagiza usawa wa chanjo ya COVID-19. Mkataba wa amani Sudan Kusini bado kitendawili kwa wakazi wa Tambura. Na nchini Tanzania vijana wajasiriamali katika mkoa wa Singida wameitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, TEHAMA kama njia mojawapo ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDG hususan kipengele cha teknolojia cha lengo namba 17 la kuimarisha mbinu za utekelezaji wa malengo na kuchochea ubia wa kimataifa

Sauti
14'29"

18 Oktoba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo baada ya kusikiliza habari kwa ufupi utasikia mada kwa kuhusu chakula cha asili kutoka Kilimanjaro nchini Tanzania.

Mwishoni mwa wiki dunia imeadhimisha siku ya chakula duniani ikibeba maudhui “Hatua zetu ndio mustakbali wetu” kwa ahadi ya kuimarisha mifumo ya chakula na kuhakikisha watu wote mahali popote walipo duniani wanapata lishe bora na mlo kamili. 

Sauti
11'10"