30 NOVEMBA 2021
Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa tuliyokuandalia hii leo ni pamoja na vipimo vya VVU vyapungua UNITAID waomba ufadhili zaidi, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linatumia mabalozi wake watoto ambao ni wachechemuzi kuhusu tabianchi kuelezea adha ambazo watoto wanapata kutokana na madhara ya tabianchi na nini wanataka kifanyike.