Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

30 APRILI 2021

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo ikiwa ni mada kwa kina Grace Kaneiya anakuletea 

-Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu ukimwi imependekeza masuala 10 ya kuzingatia kutokomeza janga hilo ifikapo 2030 na kutimiza ajenda ya SDGs.

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limeelezea kusikitishwa kwake na athari za ongezeko la mashambulizi dhidi ya wahudumu wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini

Sauti
12'20"

29 Aprili 2021

UNHCR yataka msaada zaidi kwa warundi wanaorejea nyumbani Burundi.

Afrika lazima iimarishe haraka mifumo ya chakula ili kujikwamua vyema na COVID-19, wanasema IFAD na ADB.

Na takribani watu milioni 3.4 Myanmar wanaweza kukabiliwa na njaa, inaeleza  WFP Myanmar.

Sauti
12'32"

28 Aprili 2021

Bei ya vifaa vya mtu kujipima mwenyewe VVU yashuka.

Watu milioni 29 wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi ukanda wa Sahel. 

Na, Je unawezaje kuanza upya maisha ukiwa umepoteza kila kitu?

Sauti
13'12"

27 Aprili 2021

Asante Rwanda kwa kukubali kunusuru wasaka hifadhi walio hatarini Libya, asema  Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi.

UNMISS yatoa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa vijana wa Sudan Kusini.

Na MINUSCA yasaidiana na serikali CAR kupunguza athari za kimazingira.

Sauti
11'52"

26 Aprili 2021

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP mwaka 2017 lilizindua kampeni ya bahari safi au CleanSeas kwa lengo la kushirikisha serikali, umma, mashirika ya kiraia na sekta binafsi katika kutokomeza utupaji taka kwenye maeneo ya bahari na maziwa. Tangu wakati huo kampeni hiyo imekuwa moja ya kampeni kubwa duniani ya kuondokana na taka za plastiki baharini ambapo hata watu binafsi wametumia ubunifu wao kuibuka na mbinu za kuondokana na taka hizo baharini.

Sauti
11'52"

23 Aprili 2021

Kuelekea siku ya malaria duniani Aprili 25, Grace Kaneiya akiwa Nairobi, Kenya amezungumza na Dkt. Dan James Otieno kutoka Shirika la afya ulimwenguni, WHO nchini Kenya katika programu ya malaria inayofanya kazi kwa pamoja na wizara ya afya nchini humo. Kwanza anaanza kwa kuelezea Kenya ilipofika vita dhidi ya malaria.

Sauti
11'41"

22 Aprili 2021

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kusongesha wanawake na wasichana kwenye teknolojia za Habari na Mawasiliano au TEHAMA Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka hatua zaidi zichukuliwe ili kuondoa pengo la idadi ya wanawake na wasichana kwenye TEHAMA, 

Fahamu kuhusu Alaa, mkimbizi ambaye ni mfano wa nguvu katika hali ya changamoto za maisha. 

Na WHO yazindua mkakati kutokomeza malaria katika nchi 25 ifikapo 2025.

Sauti
12'56"

21 Aprili 2021

Uamuzi dhidi ya kesi ya Floyd ungalikuwa vinginevyo, ingalikuwa kituko dhidi ya haki- Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet.

Hakuna dalili za kumalizika mzozo Tigray imeonya UNICEF.

Na chanjo dhidi ya COVID-19 imeniondoa hofu ya kuhudumia wazazi- Mkunga Uganda.

Sauti
12'50"

20 Aprili 2021

Waliofurushwa ndani ya Msumbiji wanasaidiana, lakini msaada wa haraka utahitajika wakiongezeka-UNHCR

Watoto 275 wanajikuta Mexico kila siku wakisubiri kuingia Marekani:UNICEF 

Pakistani yaanza kupatia wakimbizi wa Afghanistan kadi za kisasa za utambulisho 

Na kwenye makala, wanawake katika sanaa wanakumbana na changamoto. Vijana wasiendekeze starehe – Mama Kayai, muigizaji nguli wa Kenya. 

 

Sauti
14'13"

16 Aprili 2021

Umoja wa mataifa unaamini kuwa michezo licha ya kuwa chanzo cha kipato na afya, ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo na amani kwani kupitia michezo watu walio na tofauti mbalimbali za kijamii, wanaweza kukutana, kuondoa tofauti zao na hatimaye kushiriki katika ujenzi wa maendeleo bila kukwamishwa na tofauti zao. Ndio maana watu duniani kote wanahamasishwa kuutokomeza ugonjwa wa Civid-19, ili viwanja vya michezo vifufuke tena. Kutoka Bujumbura Burundi, washirika wetu Mashariki TV wametuandalia makala hii inayoeleza namna ambavyo michezo imefanikisha hilo nchini Burundi.

Sauti
11'59"