Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

Jarida 30 Septemba 2021

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya sekta ya bahari , janga la corona au COVID-19 limethibitisha umuhimu wa bahari na kujitolea kwa mamilioni ya mabaharia wanaofanyakazi katika sekta hiyo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Karibu usikilize jarida linaloletwa kwako na Assumpta Massoi ambapo atakujuza kwa undani taarifa hiyo na nyingine nyingi.

Sauti
12'14"

Jarida 29 Septemba 2021

Karibu usikilize jarida ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha kuhusu upotevu na utupaji wa chakula na mwenyeji wako ni mimi ASSUMPTA MASSOI. 

Miongoni mwa utakayo sikia ni pamoja na programu ya UNICEF nchini Kenya yawasaidia watoto wa kike kurejea shuleni. 

Taasisi ya kusaidia wakimbizi wandani nchini Yemen yashinda Tuzo ya UNHCR ijulikanayo kama tuzo ya wakimbizi ya Nansen. 

Sauti
14'2"

Jarida 28 Septemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo utasikia shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO na wadau wake wamezindua mkakati wa kwanza wa aina yake wa kutokomeza ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo, ugonjwa ambao unaua mamia ya maelfu ya watu kila mwaka.

pia utasikia taarifa nyingine kuhusiana na nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia Kongo - DRC 

Sauti
13'46"

Jarida 27 Septemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo utasikia sehemu ya pili ya mahojiano yaliyofanywa na Anold Kayanda na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. 

Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangalizia siku ya utalii duniani ambayo huadhimishwa leo Septemba 27.

Sauti
12'40"

Jarida 24 Septemba 2021

Ni Ijumaa ya tarehe 24 mwezi Septemba mwaka 2021 karibu kusikiliza jarida na kama ilivyo ada ya kila Ijumaa tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakuletea sehemu ndogo ya mahojiano marefu na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania baada ya hapo jana kuhutubia kwa mara yake ya kwanza katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Sauti
12'6"

Jarida 23 Septemba 2021

Ni Alhamisi  ya tarehe 23  ya mwezi Septemba mwaka 2021 siku ya tatu ya mjadala mkuu wa mikutano ya ngazi ya juu ya Umoja wa Mataifa

Miongoni utakayo sikia kwenye jarida hii leo ni pamojana Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassana ahutubia mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa, UNGA76 akizungumziamasuala kadhaa ikiwemo ushirikiano wa kimataifa na ahadi yake kwa jumuiya ya kimataifa. Halikadhalika tunakwenda Ethiopia na pia Cameroon. Makala ni Uganda na mashinani tunakutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Sauti
9'56"

Jarida 22 Septemba 2021

Ikiwa leo ni Jumatano  tarehe 22 Septemba 2021 siku ya pili ya mjadala mkuu wa mikutano ya ngazi ya juu ya Umoja wa Mataifa #UNGA76 karibu kusikiliza jarida ambapo kubwa utakalo sikia leo ni miaka 20 baada ya azimio la Durban kuhusu kupinga ubaguzi hali ipoje?. Utasikia mahojiano mbalimbali kutoka nchini Kenya na Tanzania. 

 

Sauti
14'20"

Jarida 21 Septemba 2021

Leo tarehe 21 Septemba mwaka 2021 ni siku ya amani duniani halikadhalika siku ya kwanza ya mjadala mkuu wa mikutano ya ngazi ya juu ya Umoja wa Mataifa katika makao makuu ya UN nchini Marekani.
Karibu Usikilize Jarida ambapo utasikia mengi kuhusu #UNGA76

Sauti
17'16"

Jarida 20 Septemba 2021

Katika Jarida hii leo Flora Nducha anakuletea mada kwa kina inayo mulika jinsi Umoja wa Mataifa unachagiza mashinani mifumo endelevu ya chakula ikiwa ni kuelekea mkutano wa ngazi ya juu wa umoja huo hapa New York Marekani kuhusu mifumo ya chakula.
Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs na Masuala ya Afya. 

Sauti
13'57"

Jarida 17 Septemba 2021

Ungana na Assumpta Massoi ambaye pamoja na mambo mengine anakuletea mada kwa kina inayomulika jinsi Tanzania itakavyotumia mkopo wa dharura kutoka shirika la fedha la kimataifa, IMF kwa ajili ya kukabiliana na athari za ugonjwa wa Corona au COVID-19.

Na katika kujifunza Kiswahili utapata ufafanuzi wa maana ya msemo"KINGA NA KINGA NDIPO MOTO UWAKAPO" 

Sauti
12'1"