Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

28 MEI 2021

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Leah Mushi anakuletea
-Leo ni siku ya kimataifa ya hedhi salama ujumbe ukiwa Hatua na Uwekezaji katika Hedhi salama, wakati huu ambapo suala la hedhi linachukuliwa na jamii kuwa ni ugonjwa au mkosi na hivyo kuwakosesha watoto wa kike haki ya kupata huduma ya kujisafi wakati wa mzunguko wa hedhi kila mwezi.

Sauti
12'21"

27 Mei 2021

Hii leo jaridani Leah Mushi anaanzia na habari za ulinzi wa amani ikiwa ni kuelekea siku ya walinda amani duniani tarehe 29 mwezi huu wa Mei. Atakupelekea Ghana kuangazia jinsi ilivyobainika kuwa masomo ya darasani kwa kiasi kikubwa bado hayamwezeshi kijana kujikimu maisha yake mtaani. Huko Ecuador wakimbizi kutoka Colombia wahaha kujikimu na maisha na makala leo tunapiga kambi nchini Kenya kuzungumza na mshindi wa tuzo ya kipekee ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya jinsia kwenye ulinzi wa amani. Mashinani tunakwenda Guinea, karibu!

Sauti
13'21"

26 Mei 2021

Hii leo jaridani Leah Mushi anaanzia na habari kuhusu haki za binadamu hususan wahamiaji wanaokufa maji huko bahari ya Mediteranea. Kisha Sudan Kusini ambako mradi wa UNIDO umeleta nuru na anakwenda Burundi ambako Ziwa Tanganyika maji yamefurika na kufurusha watu. Makala ni Kenya kwao Teknowgalz na mashinani ni  Zambia! karibu.

Sauti
11'11"

25 Mei 2021

Hii leo jaridani tunaanzia huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika janga la mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo jimboni Kivu Kaskazini.  Kisha tunaangazia ripoti ya UNICEF ya kwamba ukosefu wa maji ni silaha hatari zaidi kuliko hata mabomu kwa watoto. Nchini Tanzania kijana Aisha Kingu atumia mashairi kuelimisha watu kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Makala tunarejea DRC kuangazia ziara ya Mkuu wa UNFPA katika hospitali ya Panzi jimboni Kivu Kusini na tunakunja jamvi na mashinani huko Uvinza kwa wachimba madini ya chumvi.

Sauti
13'36"

21 Mei 2021

Kuelekea siku ya kimataifa ya kutokomeza ugonjwa wa Fistula ambayo huadhimishwa kila Mei 23, mwaka huu kauli mbiu ikiwa, “haki za wanawake ni haki za binadamu! Tokomeza Fistula sasa", Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani, UNFPA linasema haipaswi kuachiwa wanaokubwa na wanaoathirika kutokana na tatizo hilo kwani kila mtu anahitaji maisha yenye hadhi.

Sauti
11'

20 Mei 2021

Mitungi milioni 4 ya oksijeni yahitajika duniani kote kila siku kwa wagonjwa wa COVID-19.

Ulimwengu wajipanga kuzuia magonjwa ya mlipuko yanayoanzia kwa wanyama.

Na mjasiriamali Furaha wa DRC anaishukuru FAO na WFP akisema, "mimi na wanangu 12 twaweza kuishi."

Sauti
12'46"

19 Mei 2021

Biashara ya bidhaa yapiga jeki uchumi wa dunia wakati wa COVID-19, imesema ripoti mpya iliyotolewa na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD.

UNICEF Burundi yatoa mafunzo ya Ujuzi kwa Wasichana.

Na wakazi wakulima wa Keknaf, Bangladesh wanasema hata kabla ya kuja wakimbizi wa Rohingya, tayari wao walikuwa hoi, UNHCR imewasaidia. 

Sauti
13'4"

18 Mei 2021

UNHCR yaomba raia wa Msumbiji wanaokimbia vurugu wapewe hifadhi nchini Tanzania.

Bado tunawasaka wanakijiji  waliokimbilia msituni baada ya kuvamiwa Bahr Ole Payam, imesema UNMISS.

Na mkimbizi Marie-Reine asema programu ya rafiki imenipa ujasiri niliohitaji kuanza maisha mapya Ubelgiji.

Sauti
12'40"

17 Mei 2021

Mabadiliko ya Tabia nchi yameleta athari kote ulimwenguni, miongoni mwa changamoto zilizoletwa na adha hiyo ni pamoja na ukosefu wa mvua hali inayopelekea kuwepo na uhaba wa chakula na mahali pengine mvua kubwa zinazosababisha mafuriko na mazao kushindwa kustawi kabisa.

Sauti
10'18"

12 Mei 2021

Hali ya njaa Madagascar ni tete! UN na serikali wataka msaada wa haraka.

Hospitali bila wauguzi ni sawa na gari bila injini, anasema Muuguzi Mildred Okemo. 

Na mashirika ya UN yapambana na utapiamlo shuleni Guatemala.

Sauti
12'37"