Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 OKTOBA 2021

04 OKTOBA 2021

Pakua

Katika Jarida la Habari hii leo  kutoka Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres akifungua mkutano wa 15 wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendfeleo na biashara UNCTAD15 mjini Bridgetown Barbados ametoa wito wa kuhakikisha usawa wa biashara, uwekezaji na na kujikwamua vyema na COVID-19

-Ripoti ya kamati huru ya uchunguzi wa haki za binadamu nchini Libya imesema kuna ushahidi kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaoweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ulitekelewa nchini humo tangu 2016

-Leo ni siku ya makazi duniani , kaulimbiu ukiwa kusongesha hatua ili kujenga dunia huru bila hewa ukaa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wake amehimiza kutowasau watu wa makazi dunia dunia inapojikwamua na janga la COVID-19

-Mada yetu kwa kina leo inatupeleka visiwani Zanzibar kukutana na Bwana Salum Faki Hamadi ambaye ametunukiwa tuzo ya mwanasayansi bora kutokana na utafiti wake uliofanikisha kupatikana kwa mbegu mpya ya mpunga.

-Na mashinani leo utasikia ujumbe wa Papa Fransis kwa viongozi wa vijana wanaohudhuria Mkutano wa dunia wa Chakula, ikiwa ni sehemu ya harakati ya ulimwengu inayotaka kutumia nguvu na ubunifu wa vijana kutengeneza mustakabali mzuri wa chakula.

Audio Credit
UN News/Assumpta Massoi
Sauti
15'10"