Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

3 Novemba 2021

Karibu katika jarida ambapo utasikia kuhusu ushindi wa kijana mtanzania katika tuzo zilizotolewa leo sanjari na mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26.

Habari kwa ufupi leo zimeangazia ripoti ya uchuguzi wa masuala ya haki za binadamu huko Tigray nchini Ethiopia na baa la njaa nchiniMadagascar

Sauti
13'14"

02 Novemba 2021

Leo tarehe 02 Novemba  2021 siku ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya wanahabari  ASSUMPTA MASSOI anakuletea jaridi likizungumzia kwa undani juu ya siku hii na takwimu zilizotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni,  UNESCO pamoja na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

29 Oktoba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo kama ilivyo ada ijumaa tunakuletea mada kwa kina leo tukimulika usanifu majengo na udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi mijini kuelekea siku ya miji duniani tarehe 31 mwezi huu wa Oktoba.

Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia wito uliotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa duniani na mashirika mengine ya kimataifa tisa kuhusu maji na mabadiliko ya tabianchi. Taarrifa nyingine ni Maendeleo ya teknolojia kwa wanahabari na asasi za kiraia pamoja na mbinu bora na za kimkakati za kuwalinda watoto walioathiriwa na migogoro

Sauti
17'41"

28 Oktoba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo ASSUMPTA MASSOI anakuletea taarifa zikiwemo

-Mkutano unaohusu utafiti, sayansi teknolojia na uvumbuzi katika kukuza ushirikiano na maendeleo katika nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni sehemu ya mbio za kuyafikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs, ulioandaliwa na Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ya Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu umehitimishwa leo jijini Bunjumbura kwa kunuia kuwapa nafasi watafiti katika kukuza uchumi.

-Mradi wa chakula shuleni nchini Rwanda unatekelezwa na WFP. 

Sauti
12'6"

27 Oktoba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo tunakuletea mada kwa kina maalum kutokea Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC ikimulika michezo hususan mpira wa miguu na ulinzi wa amani ambako kumefanyika  mechi ya kirafiki kati ya Timu ya walinda amani kutoka Tanzania na wenyeji Lion Mavivi.

Pia utapata fursa ya kusikiliza habari kwa kifupi zikiangazia makubaliano ya kusambazwa dawa ya vidonge vya kutibu COVID-19 kwa wagonjwa wasio mahututi, utasikia pia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa Mataifa mashinani nchini Tanzania.

Sauti
11'38"

26 Oktoba 2021

Karibu usikilize jarida ambapo leo Assumpta Massoi amekuandalia habari mbalimbali zikiwemo

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP imeeleza kuwa ahadi mpya na zilizorekebishwa kuhusu viwango vya nchi vya kukabili mabadiliko ya tabianchi, NDCs hazijafikia lengo lililowekwa katika mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi na hivyo ulimwenguni kuwa hatarini kuwa na ongezeko la joto la angalau nyuzijoto angalau 2.7 katika karne hii.

Sauti
11'59"

25 Oktoba 2021

Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo katika mada kwa kina tutazungumzia mafunzo ya upishi wa chakula cha asili kwa watoto wakike na wakiume

Katika taarifa yetu ya Habari kwa ufupi tunaangazia mapinduzi ya kijeshi nchini Sudan na kauli zilizotolewa na viongozi wa Umoja wa Mataifa.

Sauti
11'37"

22 Oktoba 2021

Leo kama ilivyo ada ya Ijumaa tunakuletea mada kwa kina tukimulika siku ya Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa tarehe 24 mwezi huu wa Oktoba.

Pia tutakuletea taarifa ya Habari ambapo utasikia kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania kimeshambuliwa huko DRC na ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres kwa ulimwengu katika kuadimisha siku ya Umoja wa Mataifa.

Kipengele cha kujifunza kiswahili hii leo ni kutoka kwa mchambuzi kutoka Kenya akifafanua maana ya methali, "Ulivyoligema utalinywa" msemo "

Sauti
14'4"

21 Oktoba 2021

Karibu kusikilizia jarida ambapo miongoni na taarifa utakazo sikia hii leo ni pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu wanawake, amani na usalama ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati umefika kwa baraza hilo kuonesha kwa vitendo uungaji wake mkono wa harakati za wanawake katika ujenzi na uendelezaji wa amani badala ya kusalia maneno matupu. 

Sauti
13'36"