Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

1 Novemba 2021

1 Novemba 2021

Pakua

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo tunaelekea Glasgow Scotland ambako kunafanyika mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi au COP26.

Maudhui ya  mkutano huo uliofunguliwa jana Jumapili na leo kuanza rasmi mjadala wa ngazi ya juu ni manne , mosi kuzihimiza nchi kuhakikisha lengo la kutozalisha kabisa hewa ukaa ifikapo 2050 na kutozidisha nyuzi joto 1.5C linatimia, pili kuhakikisha nchi zinajenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuzilinda jamii na mazingira, tatu kuchagiza ufadhili kwa ajili ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi na nne kuzichagiza nchi kuhakikisha zinafanyakazi pamoja ili kutimiza malengo hayo.

Mkutano unashirikisha nchi na serikali, mashirika ya kimataifa, makampuni ya fedha , asasi za kiraia na wanaharakati wa sekta mbalimbali za mazingira zikiwemo za kijamii. Na miongoni mwa washiriki ni mratibu wa mradi wa kijamii wa Mikoko Pamoja kutoka Pwani ya Kenya ambaye amezungumza kwa kina na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili kuhusu mradi wao na mkutano huo

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
15'34"