Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 Oktoba 2021

21 Oktoba 2021

Pakua

Karibu kusikilizia jarida ambapo miongoni na taarifa utakazo sikia hii leo ni pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu wanawake, amani na usalama ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati umefika kwa baraza hilo kuonesha kwa vitendo uungaji wake mkono wa harakati za wanawake katika ujenzi na uendelezaji wa amani badala ya kusalia maneno matupu. 

Pia utasikia madhila wanayokutana nayo wananchi wa Sudani Kusini ambao wameishi miezi 6 na mafuriko baada ya mvua kubwa kuathiri miundombinu yote na hivyo misaada kushindwa kuwafikia.

pia utasikia harakati za kutambua vipawa miongoni mwa vijana wasiokuwa na ajira mtaani Kibera mjini Nairobi.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
13'36"