23 MACHI 2021
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea
-Watu 670,000 wamelazimika kuzikimbia nyumba zao hadi sasa huko Cabo Delgado Msumbiji kufuatia kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya raia limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.
- Leo ni siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema maji na hali ya hewa ni lila na fila havitengamani