Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 MACHI 2021

22 MACHI 2021

Pakua

Katika jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Grace Kaneiya anakuletea

-Leo ni siku ya maji duniani na Umoja wa Mataifa umesisitiza kila mtu kutambua thamani ya rasilimali hiyo muhimu ili kuhakikisha watu wote wana fursa ya kuipata kote duniani

-Nchini Sudan Kusini mpango wa Umoja wa Mastaifa UNMISS umeendesha warsha ya siku mbili Yambio na Nzara kwa ushirikiano na serikali ili kuhakikisha vijana, wanawake na jamii wanajikwamua vyema na janga la COVID-19, vita na mabadiliko ya tabianchi

-Kuelekea siku yautabiri wa hali ya hewa duniani hapo kesho Machi 23 shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO limesema bahari ni muhimu katika maisha ya watu ikiwemo uchumi na uhakika wa chakula lakini mabadiliko ya tabianchi yanatishia hilo

-Mada yetu kwa kina leo inajikita na suala la kmaji tutaelekea Uganda kusikia kuhusu juhudi za serikali kuhakikisha kila mtu anapata rasilimali hiyo na changamoto zinazowakabili wananchi.

-Na mashinani mkurugenzi mkuu wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD anaeezea umuhimu wa kila mtu kuhakikisha maji yanaenziwa kwa kila njia

Audio Credit
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration
12'33"