Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

10 Machi 2021

10 Machi 2021

Pakua

Leo Jumatano ya Machi 10, 2021 Flora Nducha anaanza na ripoti kutoka Kenya ambako chanjo imeanza kutolewa dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19. Kisha anakwenda nchi jirani ya Tanzania ambako Umoja wa Mataifa kupitia kituo chake cha biashara, ITC, umeleta nuru kwa wanawake wajasiriamali wanaokamua chikichi kuwa mafuta ya mawese huko Kigoma. Kutoka Tanzania ni Sudan Kusini ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Bangladesh wanajenga barabara katika mazingira magumu. Makala ni nafasi ya vijana wanawake katika kusongesha haki za ardhi na mashinani tunabisha hodi shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO. Karibu

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'7"