Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 Machi 2021

11 Machi 2021

Pakua

Hii leo jaridani ikiwa ni mwaka mmoja tangu shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO litangaze ugonjwa wa Corona au COVID-19 ni janga la afya duniani, tunaanzia nchini Uganda ambako chanjo dhidi ya ugonjwa huo imeanza kutolewa kwa wahuudumu wa afya na wafanyakazi wengine muhimu walio mstari wa mbele. Tutasalia huko huko Uganda kwenye makazi ya wakimbizi  ya Bidibidi ambako walipata ugeni kutoka kwa Kamishna Mkuu wa wakimbizi duniani, Filippo Grandi. Huko Yemen nako tunabisha hodi kwa kuwa mapigano nchini humo yamesababisha watu waishi maisha dhalili na Mkurugenzi Mkuu wa WFP David Beasley amekutana uso kwa uso na wayemen. Makala tunamulika mboga na matunda umuhimu wake mwilini na mashinani tunabisha hodi Syria ambako miaka 10 ya mapigano yamemfanya mama mwenye familia ya watu 9 akiwaza na kuwazua maisha yao ya ukimbizi yataisha au ndio yatasalia kama yalivyo sasa? Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'13"