Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 MACHI 2021

16 MACHI 2021

Pakua

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo  Grace Kaneiya anakuletea 

-Somalia imefuata nyayo za  nchi zingine za Afrika na kuanza kampoeni ya chanjo dhidi ya COVID-19 baada ya kupokea shehena kupitia mkakati wa COVAX

-Mwaka mmoja baada ya kuzinduliwa kwa mfuko wa kiamataifa wa mshikamano kwa ajili ya COVID-19 WHO inasema umefanya mambo mengi lakini inawasihi wahisani kuendelea kuutunisha 2021

-Miaka 10 ya vita vya Syria shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema nusu ya raia wote wa Syria wamekimbia makwao na madhila bado yanawazogoma

-Makala yetu leo inatupeleka Kenya kuzungumza na mwanamke bondia na mama wa watoto wawili

-Mashinani tuko Mali kwa mlinda amani wa Umoja wa Mataifa mwanamke anayesema alishauriwa asijiunge na jeshi kwa kuwa ni mwanamke.

Audio Credit
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration
12'40"