Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 MACHI 2021

23 MACHI 2021

Pakua

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Watu 670,000 wamelazimika kuzikimbia nyumba zao hadi sasa huko Cabo Delgado Msumbiji kufuatia kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya raia limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

- Leo ni siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema maji na hali ya hewa ni lila na fila havitengamani

-Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNFPA, Dkt. Natalia Kanem amekamilisha ziara yake ya siku tano nchini Sudan na kusema , ameshuhudia jinsi uwekezaji kwa wanawake na vijana umekuwa msaada mkubwa hasa katika sekta ya afya ya uzazi.  

-Makala yetu inatyupeleka Tanzania ambapo Ahimidiwe Olotu wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC jijiin Dar es salaam  anazungumza na Salha Kibwana, wa mpango wa Her Africa kuhusu shirika hilo linalosaidia wasichana shuleni kijamii na kiuchumi.

-Na mashinani tutaungana na Dkt. Adnan Mustafa, daktari wa watoto katika hospitali ya kitaifa Kenya ya Kenyatta ambaye  ni miongoni mwa watu waliopokea chanjo dhidi ya virusi vya corona au COVID-19

 

Audio Credit
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration
13'54"