Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 Machi 2021

12 Machi 2021

Pakua

Hii leo jaridani Ijumaa ya tarehe 12 machi 2021 Flora Nducha anakuletea mada kwa kina ikibisha hodi huko Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kukutana na familia ambayo inamletea mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minane baada ya kumuokoa msituni wakati wa mashambulizi kutoka kwa waasi wa kikundi cha ADF. Leo pia ni wasaa wa kujifunza Kiswahili ambapo methali isemayo La kuvunda halina ubani itamulikwa na mchambuzi wetu kutoka BAKIZA. Lakini kwanza kabisa ni habari kwa ufupi inayoletwa kwako na Anold Kayanda akianzia Syria janga la elimu ndani ya muongo mmoja wa vita, kisha Somalia ambako uhaba wa mvua unatishia ukame huku shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO likitamatisha habari hizo kwa taarifa kuhusu nchi 22 za Afrika ambazo tayari zimeshapokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19. Karibu!

Audio Credit
Flora nducha
Audio Duration
11'55"