Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

16 Desemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa utakayo sikia leo ni kuhusiana na utapiamlo Garissa nchini Kenya, viongozi wa dini watembelea wakimbizi wa ndani nchini Sudan Kusini na Mtumishi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania ambaye amekuwa akifanya kazi ya udereva kwa miaka zaidi ya 20 amezungumzia miaka 75 ya UNICEF. 

Kwa habari hizo na nyingine nyingi ungana na Flora nducha . 

Sauti
14'22"

15 Desemba 2021

Karibu kusikiliza jarida, tunakuletea mada kwa kina kutoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, huko tunaangazia ujio wa kikosi kipya cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania ambacho kinachukua nafasi ya kikosi kingine kutoka Tanzania vilevile ambacho kimemaliza muda wake katika shughuli za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.

Pia utaapata kusikiliza habari kwa ufupi zikiangazia mwenendo wa janga la Corona au COVID-19 na masuala mengine ya Umoja wa Mataifa. 

Sauti
11'8"

14 Desemba 2021

Hujambo na karibu kusikiliza jarida msomaji wako ni Flora Nducha anayekuletea mambo kadha wa kadha ikiwemo

Ripoti inayoonesha kuongeza kwa njaa barani Afrika huku ukanda wa Afrika Mashariki ukiongoza kwa asilimia 44. 

Wakimbizi wa DRC walioko nchini Uganda wameanza kurejea makwao kwa hiyari.

Sauti
13'9"

13 Desemba 2021

Karibu kusikiliza jarida, kila Jumatatu tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunaangazia Kikosi cha wanajeshi kutoka Uingereza kinachohusika na upelelezi wa masafa marefu au LRRG chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka amani nchini Mali, MINUSMA. 

Lakini pia utapata fursa ya kusikiliza habari kwa ufupi leo zikiangazia masuala mbalimbali ikiwemo jukwaa lililozinduliwa leo la kuwasaidia watoto wanaugua saratani kupata dawa katika nchi za kipato cha kati na cha chini. 

Sauti
10'34"

10 Desemba 2021

Ni ijumaa ya tarehe 10 mwezi Desemba mwaka 2021 siku ya haki za binadamu duniani, karibu tuwe sote katika mada kwa kina ambayo leo inaangazia haki za kisheria nchini Uganda, wananchi, polisi na kamisheni ya haki za binadamu wana yapi ya kusema.

Lakini pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia siku hii ya haki za binadamu na ushauri uliotolewa na WHO kwa nchi zenye kipato cha chini na cha kati kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza. 

 

Sauti
12'5"

09 Desemba 2021

Karibu kusikiliza jarida, mwenyeji wako ni Flora Nducha anayekujuza kwa undani kuhusu. 

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imesema janga la COVID-19 limeleta hali mbaya zaidi kwa watoto kuwahi kushuhudiwa katika historia yake ya miaka 75 nakuzitaka nchi kuongeza juhudi kuwanusuru watoto.

Sauti
13'15"

08 Desemba 2021

Ni Jumatano ya tarehe Nane mwezi Desemba mwaka 2021, karibu tuwe sote katika mada kwa kina ambayo leo Utamsikia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali wa Tanzania ambaye yupo hapa jijini New York Marekani, Kafata nini? karibu usikilize.

Sauti
13'20"

07 Desemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa utakayo sikia leo ni WHO yakataza mtu aliyepona COVID-19 kumchangia damu mgonjwa anayeugua COVID-19 pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani UNEP leo limewatangaza washindi wanne wa tuzo yake ya juu kabisa ya mazingira ijulikanayo kama “champions of the Earth Award” kwa mwaka 2021. 

Jiunge na Flora Nducha kupata undani wa taarifa hizo na nyingine nyingi 

Sauti
13'34"

06 Disemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo kuelekea siku ya haki za binadamu ambayo huadhimishwa kila tarehe 10 ya mwezi wa 12, tunakuletea vipindi mbalimbali vinavyoeleza umuhimu wa kutekeleza haki za binadamu. Leo tunaangazia haki ya kuishi na kutokubaguliwa ya watu wenye ulemavu.

Assumpta Massoi anatupeleka nchini Tanzania katika mkoa wa Mwanza ulioko kandokando mwa Ziwa Victoria, kaskazini magharibi mwa nchi kuona juhudi zinazofanywa na jamii kupambana na imani potofu zinazosababisha watu wenye ualbino kuishi kwa mashaka.

 

Sauti
10'33"

03 Desemba 2021

Karibu kusikiliza jarida hii leo tukikuletea mada kwa kina kutokea nchini Tanzania kuhusu mapokeo ya uamuzi wa serikali kuwarejesha shuleni watoto waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo  ujauzito.

Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu ambayo ni leo na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa siku hii pamoja na habari kutoka Afghanistan na Ethiopia. 

Sauti
12'25"