Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

na hatimaye

Alkhamisi tarehe 23 Agosti iliadhimishwa na Shirika la UM juu ya Ilmu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu juu ya Ukomeshaji wa Utumwa na Biashara ya Utumwa Duniani, hali ambayo Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Koichiro Matsuura alisisitiza athari zake bado zinaendelea kupalilia dhulma, uonevu na utenguzi wa haki za kibinadamu katika sehemu kadha wa kadha za dunia sasa hivi.

Kuongezeka kwa ghasia dhidi ya vyombo vya habari huko Somalia

Kwa mara nyingine vyombo vya habari huru huko Somalia vyapoteza waandishi habari wawili mwishoni mwa wiki iliyopita. Ali Iman Sharmarke muanzilishi na mwenyekiti wa kituo mashuhuru cha redio na televisheni pamoja na mwandishi habari wa kipindi mashuhuri Mahad Ahmed Elmi wa kituo hicho hicho, waliuliwa karibu wakati mmoja huko Mogadishu.

Hapa na pale

.Utafiti mpya ulofanya na afisi ya haki za binadam ya UM unaonesha kwamba jamii huko kaskazini ya Uganda wanawalaumu wote wanajeshi wa serekali na wapigganji wa waasi wa Lord Resistance Army LRA kwa ukatili ulotendeka wakati wa zaidi ya miaka 20 ya vita na wanataka walohusika kuhukumiwa na kuwajibika.

Siku ya Kimataifa ya Wazawa

Karibu wazawa milioni 370 kote duniani wanaendelea kubaguliwa, kutengwa na kuishi katika hali ya umaskini kabisa na ghasia, Katibu Mkuu wa UM bw Ban Ki-moon, alitoa mwito wa kuchukuliwa hatua za dharura kukabiliana na matatizo hayo.