Skip to main content

na hatimaye

na hatimaye

Alkhamisi tarehe 23 Agosti iliadhimishwa na Shirika la UM juu ya Ilmu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu juu ya Ukomeshaji wa Utumwa na Biashara ya Utumwa Duniani, hali ambayo Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Koichiro Matsuura alisisitiza athari zake bado zinaendelea kupalilia dhulma, uonevu na utenguzi wa haki za kibinadamu katika sehemu kadha wa kadha za dunia sasa hivi.