Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu apongeza kufanyika uchaguzi mkuu kwa amani Sierra Leone

Katibu Mkuu apongeza kufanyika uchaguzi mkuu kwa amani Sierra Leone

Akipongeza kufanyika kwa ufanisi uchaguzi wa kwanza wa rais na wa bunge huko Sierra Leone tangu kuondoka kwa walinda amani wa UM 2005, Katibu Mkuu Ban Ki-moon, amewahimiza wananchi wa taifa hilo la Afrika Magharibi, kuendelea kua watulivu wakati kura zinaendelea kuhesabiwa.

Bw Ban alifurahishwa kusikia uchaguzi ulifanyika kwa amani na watu kujitokeza kwa wingi na aliwapongeza wananchi wa Siera Leone kwa kuonesha nia yao ya kuimarisha amani na demokrasia nchini mwao. Katibu Mkuu alipongeza pia tume ya taifa ya uchaguzi na idara za usalama kwa kuanda mipango ya usalama na utawala kurahisisha utaratibu kamili wa uchaguzi. Uchaguzi huko Sierra leone ulofanyika jumamosi iliyopita ni wa pili tangu kumalizika kwa vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka kumi vilivyo malizika 2002.