Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hali ya mgogoro katika Mashariki ya Kati.

Alkhamisi KM Kofi Annan aliwakilisha mbele ya Baraza la Usalama, katika kikao cha hadhara, ripoti maalumu kuhusu hali katika Mashariki ya Kati, taarifa ambayo inaelezea matokeo ya juhudi za ujumbe wa maofisa watatu wa vyeo vya juu wa UM, waliozuru Mashariki ya Kati karibuni, kwa madhumuni ya kutafuta taratibu za kuridhisha kusitisha mapigano haraka na kuwasilisha suluhu inayokubalika na wote wahusika na mgogoro huo.~

UNEP yazingatia hifadhi ya mikoko katika Bahari ya Pasifiki.

Shirika la UNEP limetangaza kwamba utafiti ulioendelezwa karibuni kuhusu hali ya mikoko katika Bahari ya Pasifiki umethibitisha ya kuwa kunahitajika kuchukuliwa hatua za haraka za pamoja, kimataifa, kuhifadhi uchumi wa mfumo muhimu wa ikolojia ya eneo hilo. Mabadiliko ya hali ya hewa yalionekana kukithirisha kima cha usawa wa bahari na kuhatarisha mazingira maumbile ya eneo.