Kuongezeka kwa ghasia dhidi ya vyombo vya habari huko Somalia

Kuongezeka kwa ghasia dhidi ya vyombo vya habari huko Somalia

Kwa mara nyingine vyombo vya habari huru huko Somalia vyapoteza waandishi habari wawili mwishoni mwa wiki iliyopita. Ali Iman Sharmarke muanzilishi na mwenyekiti wa kituo mashuhuru cha redio na televisheni pamoja na mwandishi habari wa kipindi mashuhuri Mahad Ahmed Elmi wa kituo hicho hicho, waliuliwa karibu wakati mmoja huko Mogadishu.

Michele:

Eric Laroche anatoa mwito wa kuchukuliwa hatua thabiti kuhakikisha uhuru na usalama wa vyombo vya habari, kumekuwepo na muongezeko wa mashambulizi hivi karibuni dhidi ya vyombo vya habari huko Somali yanayofikisha idadi ya waandishi habari walouliwa kufikia sita nchini humo mwaka huu. Laroche anatoa mwito kwa mamlaka na makundi yote nchini humo kuheshimu haki za wote wenye kutoa maoni bila ya kuingiliwa kati na wanaojaribu kutoa habari zisizopendelea upande wowote kwenye vyombo vya habari.

Mwaka jana redio ya UM ilizungumza na mwandishi habari Elmi aliyezungumza hisia za matumaini makubwa ya HornAfrik akisema wakati huo, kuwapatia wananchi chombo cha kuwasiliana na kubadilishana mawazo kuna wahamasisha watu.

Elmi: It electrifies..

Inahamasisha kwa sababu wakati watu wanasema kile kilicho fikirani mwao juu ya masuala moto moto mambo yanayo wakera kila mtu na hata mara nyingine mapendekezo na mwazo yanaweza kutanzuliwa watu wanapenda sana. Kila mtu anasema lo huyu mtu ameeleza anacho fikiri kidhati.

AALakini kwa bahtai mbaya sauti hiyo imenyamazishwa. Na hakuna aliyetangaza kuwajibika na ukatili huo.

Na hali hiyo inatokea wakati kuna shida ya kupata nchi zaidi kuchagia kikosi cha kulinda amani cha Jumuia ya Afrika huko Somalia AU. Hadi hivi sasa ni Uganda pekee iliyopeleka wanajeshi wake huko Somalia na balozi maalum wa Umoja wa Mataifa Francois Lonseny Fall, ana jukumu lisilo rahisi la kutafuta suluhisho la kisiasa kutanzua mzozo wa nchi hiyo ambayo haikua na serekali kuu tangu kunagushwa kwa Rais Siade Barre 1991. Akizungumza na waandishi habari Bw Fall aliwakumbisha kwamba AU inataka kuwapeleka wanajeshi eflu nane kwa ajili ya kikosi cha AMISOM.

Fall: We have 1700 all form Uganda

AAlakini hadi hivi sasa tuna wanajeshi 1 700 wote kutoka Uganda tunawatarajia 1 500 kutoka Burundi lakini ni kwa sababu ya ukosef wa msaada wa kifedha na kiufundi ndiyo imechelewesha kupelekwa wanajeshi wa Burund. Tunataraji pia wanajesh kutoka Nigeria na Ghana.

AA Lakini inavyo onekana kuna wasi wasi wa kupeleka wanajeshi zaidi kukamilisha idadi ya AMISOM kwa sababu ya kuendelea mapigano nchini humo. Na Bw Fall anasema, kuna nchi nyenginezo zina wasi wasi kwa vile hakuna hata makubaliano ya kusitisha mapigano na hivyo inakua vigumu kabisa. Wanadiplomasia wa kiafrika wanasema kwamba kuleta amani Somalia haijalazimu kuachiwa Jumuia ya afrika pekee bali baraza la usalama lina wajibu wa mbele kuleta amani na usalama duniani.