Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la pongeza mazungumzo ya Arusha juu ya Darfur

Baraza la Usalama la pongeza mazungumzo ya Arusha juu ya Darfur

Baraza la Usalama la UM limepongeza maendeleo yaliyopatikana wakati wa mazungumzo ya awali, wiki iliyopita kati ya makundi ya waasi wa Darfur, na Baraza limetoa mwito kwa pande zote kuchukua hatua za dhati ili kuweza kupatikana amani ya kudmu huko Magharibi ya Sudan.

Mazungumzo hayo ya Arusha yaliyosimamiwa kwa pamoja na wajumbe wa UM na Jumuia ya Afrika AU kwa ajili ya Darfur, Jan Eliasson na Salim Ahmed Salim, yalimalizika kwa viongozi wa waasi walohudhuria kukubaliana na mpango wa kufikia amani ulopendekezwa na wajumbe maalum na kwamba watawaslisha mapendekezo ya pamoja juu ya kugawanya madaraka, pamoja na rasil mali masuala ya usalama na kijami. Na kwamba watafanya kazi pamoja kujaribu kutafuta suluhisho la kisiasa kwa mzozo huo uloangamiza jimbo hilo la magharibi la Sudan tangu 2003.