Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Raisi wa BK asema madai ya kumzuia mwakilishi wa Israel kuhutubia ni "uongo uliodhamiria mabaya"

Raisi wa Baraza Kuu la UM, Miguel D’Escoto ameshtumu leo, kwa kupitia msemaji wake, ya kwamba madai yalioenezwa kwenye vyombo vya habari ya kutomruhusu mjumbe wa Israel kuhutubia kwenye Baraza Kuu kuadhimisha miaka 60 ya Azimio la Mwito wa Kimataifa juu ya Haki za Binadamu, ni madai ambayo, na namnukuu hapa, “yaliojaa tetesi za uongo hakika uliodhamiria maovu.”

Kilimo cha umwagiliaji maji ndio ufunguo wa kudhaminia akiba ya chakula Afrika

Kilimo cha umwagiliaji maji na usimamizi bora wa matumizi ya maji ndio “mambo muhimu” yatakayosaidia kukuza na kuimarisha akiba ya chakula katika mataifa ya Afrika, alisisitiza Jacques Diouf, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika kla UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) kwenye hotuba yake ya ufunguzi, alioitoa leo hii kwenye mkutano wa siku tatu ulioanza Sirte, Libya, kuzingatia Udhibiti wa Maji kwa Kilimo na Nishati katika Afrika.

Ustawi wa kilimo cha mbatata wahatarishwa na migogoro ya uchumi duniani

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limechapisha ripoti mpya iliotolewa Ijumatatu inayohadharisha ya kwamba uzalishaji uliostawi wa mbatata/viazi katika mataifa yanayoendela huenda ukazorota kwa sababu ya kupwelewa kwa shughuli za uchumi duniani, kadhia ambayo husababisha upungufu wa uekezaji kwenye kilimo, ukosefu wa biashara katika soko la kimataifa na ukosefu wa uwezo wa kupata mikopo kwa wakulima.

ICG itafanyisha mazungumzo maalumu Makao Makuu kufufua mipango ya amani Usomali

Kundi la Kimataifa juu ya Mawasiliano ya Amani (ICG) linalojumuisha mashirika na nchi wanachama zilizojihusisha na mpango wa amani kwa Usomali, likiongozwa na Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali Ahmedou Ould Abdallah, linatazamiwa kukutana kesho Ijumanne hapa Makao Makuu kwenye kikao cha ngazi za juu, kusailia suluhu juu ya masuala yanayohusu usalama, hali ya kisaiasa na misaada ya kiutu inayohitajika kurudisha utulivu na amani Usomali. ~

Hapa na Pale

Ofisi ya UM ya Mratibu Maalumu juu ya Mpango wa Amani Mashariki ya Kati (UNSCO) imeripoti kinu cha taa/umeme cha Tarafa ya Ghaza, ambacho hukidhi baadhi ya mahitaji ya eneo, kimefungwa kukhofia kisije kikaharabika zaidi kutokana na kuwashwa na kuzimwa mara kwa mara, kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vya kuendeshea mtambo wa umeme. Baadhi ya sehemu za Ghaza hukoseshwa umeme kila siku kwa saa 12, na maeneo mengine hukosa umee kwa saa 4 kila siku. UNSCO imeripoti pia malori 81 yaliruhusiwa Ijumatatu kuingia eneo la Tarafa ya Ghaza, kutokea Israel, yakijumlisha pia malori 20 ya mashirika ya UM yanayohudumia misaada ya kiutu. Malori ya mashirika ya UM yalibeba shehena ya unga, maziwa, madawa na vitu vyengine kukidhia mahitaji ya watumishi wao.