Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Ukosefu wa usawa duniani unadhulumu umma afya bora, UM wabainisha

Tume maalumu ya watu 13, iliojumlisha wataalamu, viongozi waliostaafu wa mataifa pamoja na mawaziri wa afya kwenye ripoti iliowasilishwa Alkhamisi waliafikiana, baada ya kuendeleza uchunguzi wa miaka mitatu, kwamba "ukosefu wa haki za kijamii ni tukio linalosababisha vifo vya watu ulimwenguni kwa kiwango kikubwa kabisa".

Hapa na Pale

KM BanKi-moon amepongeza taarifa ya Serikali ya Zimbabwe kuondosha vikwazo dhidi ya operesheni za ndani ya nchi za mashirika yasio ya kiserkali na yale mashirika ya binafsi ya kujitolea. Alisema KM maendeleo haya ya kutia moyo yatasaidia kuhakikisha misaada ya kiutu ya kimataifa itagawiwa umma wa Zimbabwe bila upendeleo ili kunusuru maisha na kuwapatia kinga boraya afya.~

UNAMID yajaribu kurudisha hali ya matumaini kwa IDPs wa Darfur

Rodolphe Adada, Mjumbe Maalumu wa Pamoja wa UM/UA kwa Darfur ameamrisha kupeleka kwenye kambi ya Kalma ya wahamiaji wa ndani katika jimbo la Darfur Kusini, timu ya maofisa wa mapolisi, washauri wa kijeshi, wahudumia haki za kibinadamu na vile vile maofisa wanaohusika na masuala ya kiraia kufanya uchunguzi juu ya tukio liliojiri mapema wiki hii huko ambapo wahamiaji wa ndani (IDPs) 31 waliuawa baada ya mapambano na vikosi vya usalama vya Sudan.

Bassole amewasili Darfur kuanza rasmi kazi

Mpatanishi Mkuu wa Pamoja wa UM-UA kwa Darfur, Djibril Bassole amewasili kuanza kazi rasmi katika El Fasher hii leo, mji mkuu wa Darfur Kaskazini na ambapo pia yalipo makao makuu ya UNAMID. Baadaye Bassole ataelekea Nyala na El Geneina, miji mikuu ya Darfur Kusini na Magharibi.~~