Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Waziri wa Nchi za Kigeni wa Urusi kuliambia BK 'usalama wa Abkhazia na Ossetia Kusini sasa utadhaminiwa kihakika'

Majadiliano ya jumla kwenye kikao cha Baraza Kuu cha wawakilishi wote bado yanaendelea Makao Makuu na yameingia siku ya sita.~~ Lakini kwenye mjadala wa siku ya tano, Ijumamosi, Waziri wa Nchi za Kigeni wa Shirikisho la Urusi, Sergey V. Lavrov alwaambia wawakilishi wa kimataifa usalama wa majimbo yaliojitenga katika Georgia, ya Abkhazia na Ossetia Kusini, sasa utadhaminiwa kihakika baada ya taifa lake kutambua uhuru wa maeneo hayo. ~

Hapa na Pale

Ndege ya helikopta iliokodiwa na UM kuhudumia Vikosi vya Mchanganyiko vya UM/UA kwa Darfur (UNAMID) iliripotiwa kuanguka na kuharibiwa kabisa ilipoanza kuruka kutoka Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini. Wahudumu wanne wa helikopta hiyo walifariki. Marie Okabe, msemaji mshiriki wa KM, aliwaambia waandishi habari ya kwamba ripoti za awali zilizopokewa na UM zimethibitisha ndege yote iliteketea. Taarifa ziada zinatarajiwa kutangazwa baada ya UNAMID kumaliza uchunguzi kamili kuhusu ajali.~

Syria imeambia UM mazungumzo na Israel yana matumaini ya amani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Walid Al-Moualem leo Ijumamosi aliwaambia wajumbe wa kimataifa waliohudhuria kikao cha Baraza Kuu cha wawakilishi wote ya kwamba mazungmzo yasiodhahiri yanayofanyika sasa na Israel, yanayoongozwana Uturuki, yana uwezo wa kuandaa amani kati yao pindi vipengele fulani vitakamilishwa.

Mizozo ya kimataifa karne ya sasa yahitajia suluhu za washiriki wingi, inasisitiza Ujerumani

Waziri wa Masuala ya Nchi za Kigeni wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeir Ijumaa alilwaambia wajumbe waliohudhuria kikao cha 63 cha Baraza Kuu hapa Makao Makuu ya kwamba matatizo muhimu yanayokabili ulimwengu wetu kwa sasa hayatoweza kupatiwa suluhu ya kuridhisha mpaka pale nchi zote za ulimwengu zitakapochangisha juhudi zao kipamoja kuyatatua masuala hayo – kuanzia masuala ya kurudisha utulivu katika Afghanistan na Pakistan, kuimarisha amani Mashariki ya Kati na kupunguza urimbikizaji na pia matumizi ya silaha za mauaji ya halaiki ulimwenguni.

Hapa na Pale

Baraza la Usalama limepitisha, kwa kauli moja, azimio linaloitaka Iran kutekeleza, haraka, kwa ukamilifu yale maazimio yaliopita ya Baraza yalioshurutisha kusitishwa shughuli za kusafisha madini ya yuraniamu halisi inayotumiwa ama kuzalisha nishati ya umeme au silaha, na kuitaka ishirikiane nawakguzi wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA). ~~

Uhakika wa majadiliano ya jumla ya Baraza Kuu

Ijumaa wingi wa viongozi wa dunia, kwenye majadiliano ya wawakilishi wote yaliofanyika katika ukumbi wa Baraza Kuu, yalioingia siku ya tano, walikubaliana juu ya umuhimu wa kuikabidhi UM madaraka ya kusimamia juhudi za kusuluhisha mizozo iliojiri hivi sasa kwenye soko la kimataifa, kuhusu mifumko ya bei za chakula na kupanda kwa kasi kwa bei za nishati pamoja na matatizo ya fedha katika soko la kimataifa.

Mapitio ya majadiliano ya jumla katika kikao cha 63 cha Baraza Kuu

Mnamo siku ya tatu, na ya nne, ya majadiliano ya wawakilishi wote kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la UM, ambayo yalifanyika Alkhamisi na Ijumaa, wingi wa viongozi wa kutoka Afrika, hususan wale waliowakilisha mataifa ya kusini ya Sahara, walishtumu na kulaumu juu ya namna mifumko ya bei za chakula na nishati kwenye soko la kimataifa zilivyoathiri na kuhariibu shughuli zao za kiuchumi na jamii.~