Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

UNHCR ina wahka juu ya usalama wa wahamiaji wa ndani katika JKK

UM umeripoti kuwa na wasiwasi mkuu juu ya usalama wa umma uliopo kwenye eneo la vurugu karibu na Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK). Ron Redmond Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) aliwaambia waandishi habari Geneva Ijumaa kwamba wamepokea habari za kushtusha kuhusu hali ya wahamiaji wa ndani waliopo Rutshuru, mji wa Kivu Kaskazini uliopo kilomita 90 kutoka Goma.~~

OCHA inasema hali Goma ni ya kubadilika

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) inasema hali katika Goma ni yenye kubadilika na haina uhakika, na UM itabidi usubiri zaidi mpaka pale utulivu utakaporejea kwa wao kuweza kuwapelekea posho ya chakula wahamiaji wa ndani 50,000 waliong’olewa makazi kwa sababu ya mapigano.~

Kamati ya haki za walemavu kuteuliwa rasmi

Asubuhi ya leo, kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York, kikao cha awali cha Mataifa Yalioridhia na Kuidhinisha Mkataba wa Haki za Watu Walemavu kilikutana rasmi kuchagua wajumbe 12 wa kutumikia Kamati juu ya Haki za Watu Walemavu. ~

Hapa na Pale

KM alipokuwa New Delhi, Bara Hindi Ijumaa aliwaambia waandishi habari kama katika siku mbili ziliopita alifanikiwa kufanya mazungumzo ya hali ya juu, ya ushauri juu ya hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), na Raisi Paul Kagame wa Rwanda, Raisi Joseph Kabila wa JKK na Raisi Jakaya Kikwete wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa UMwa Afrika. Kadhalika KM alisema alizungumza na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Jean Ping, Waziri wa Masuala ya Nchi za Kigeni wa Marekani, Condoleeza Rice,

Uchambuzi wa Mratibu wa UM juu ya Udhibiti wa Homa ya Mafua Kimataifa

Karibuni, Dktr David Nabarro, Mratibu wa UM juu ya Udhibiti Bora wa Mripuko wa Maradhi ya Homa ya Flu Ulimwenguni alikutana na waandishi habari wa kimataifa waliopo katika Makao Makuu ya UM kuelezea maendeleo katika maandalizi ya kukabiliana na janga hili. Alitahadharisha ya kwamba wataalamu wa afya wanaashiria janga la maradhi ya homa ya mafua ya ndege huenda likaripuka ulimwenguni wakati wowote, kwa sababu ya mwelekeo wa kihistoria juu ya duru ya mifumko ya maradhi haya katika ulimwengu.

UM yaomboleza mauaji ya wafanyakazi wawili Usomali

Mark Bowden, Mratibu Mkazi wa Misaada ya Kiutu kwa Usomali amethibitisha hii leo, kutokea Nairobi, ya kwamba watumishi wawili wa UM waliuawa Ijumatano asubuhi kwenye mji wa Hargeisa, Usomali Kaskazini pale majengo ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) yaliposhambuliwa na watu waliojitolea mhanga, waliotumia gari liliokuwa na viripuzi.

Taarifa ziada za huduma za kihali za UM katika Goma

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetupatia taarifa mpya kuhusu juhudi za UM katika ugawaji wa misaada ya kihali katika Goma na maeneo jirani, hususan kwa wale wahamiaji muhitaji walioathirika na mapigano yaliozuka karibuni baina ya vikosi vya Serikali na makundi ya waasi wa CNDP.