Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kushoto) na Thomas Bach, Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), mjini Paris kabla ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya Paris 2024.
© IOC/Greg Martin

Pongezi IOC kwa kuendelea kujumuisha wanariadha wakimbizi kwenye Olimpiki- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko Paris Ufaransa kuhudhuria ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto mwaka 2024 amezungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach na kuipongeza kamati hiyo kwa kuendelea kuwajumuisha wakimbizi wanamichezo. 

Audio Duration
1'50"
Wahudumu wa afya Sierra Leone wakifundishwa matumizi ya vifaa vya kielektroniki katika usimamizi na ufuatiliaji wa magonjwa na afya.
WHO/Saffea Gborie

WHO Afrika yafanikiwa kuboresha afya ya umma barani Afrika

Jitihada za pamoja za kukabiliana na changamoto za afya ya umma zinazidi kuboresha upatikanaji na utoaji wa huduma za afya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kanda ya Afrika kwa kushirikiana na nchi wanachama na washirika wake linaendelea kutimiza ajenda yake ya mabadiliko ili kuimarisha mifumo ya afya na kuongeza misaada kwa nchi katika ukanda wa Afrika.

Audio Duration
2'1"
Mitaa ya Dhaka, Bangladesh.
Austin Curtis/Unsplash

Bangladesh: Kamishna Türk alaani msako dhidi ya waandamanaji ataka sheria zizingatiwe 

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk  hii leo ameitaka serikali ya Bangladesh haraka iweke wazi na kwa kina maelezo kuhusu msako wa wiki iliyopita dhidi ya waandamanaji wakati huu ambapo kuna taarifa za kutishi kuhusu ghasia na wakati huo huo ihakikishe vyombo vya usalama vinazingatia sheria na maadili ya kimataifa ya haki za binadamu.