Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO kutangaza takwimu mpya za janga la kipindupindu Zimbabwe

WHO kutangaza takwimu mpya za janga la kipindupindu Zimbabwe

Shirika la Afya Duniani (WHO) leo Ijumaa limetoa takwimu mpya kuhusu waathirika wa kipindupindu katika Zimbabwe.

“Kuanzia tarehe 11 Disemba jumla ya wagonjwa 16,700 waliripotiwa kupatwa na maradhi ya kipindupindu katika Zimbabwe, na kati ya idadi hiyo wagonjwa 792 walishafariki. Hicho ni kiwango cha asilimia 4.7 ya vifo. Kwa WHO kuweza kuthibitisha janga hili limedhibitiwa kihakika, kiwango cha vifo kwa kulingana na jumla ya wagonjwa, kinatakiwa kiteremke chini ya asilimia moja. Wingi wa watu waliopatwa na maradhi wamekutikana zaidi katika eneo la mji wa Harare, ambapo ndipo paliposajiliwa wagonjwa 842, na vifo 189. Vile vile kumekutikana wagonjwa wa kipindupindu kwenye eneo la Beit Bridge, linalopakana na Afrika Kusini, na katika eneo la mpaka na Msumbiji la Modzi. Mripuko wa idadi hii ya wagonjwa wa kipindupindu katika Zimbabwe ni mkubwa sana, na haujawahi kushuhudiwa kihistoria hapo kabla. Hivi sasa WHO inahitajia mchango wa dola milioni sita ili kuhudumia shughuli za kudhibiti kipindupindu nchini Zimbabwe katika mwezi ujao.”