Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

'UM uliopoa' kutunza mazingira Makao Makuu

Kuanzia Ijumaa tarehe mosi Agosti, UM utatekeleza mradi maalumu kwenye majengo ya Makao Makuu yaliopo New York, kwa matarajio ya kuongeza akiba ya fedha za matumizi na kutunza mazingira. Hatua hii inachukuliwa kwa kulingana na juhudi za kimataifa za kukabiliana na matatizo yanayotokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, na UM imeamua kuongoza kwenye juhudi hizi kwa vitendo.

WIPO imeripoti kuongezeka duniani kwa maombi ya hakimiliki

Shirika la UM juu Ya Hakimiliki za Taaluma Duniani (WIPO) kwenye Ripoti ya 2008 kuhusu maombi ya umiliki wa uvumbuzi wa vitu vunavyotengenezwa, kuuzwa na kutumiwa na umma wa kimataifa, imebanisha kwamba kumepatikana muongezeko mkubwa wa maombi hayo, katika miaka ya karibuni, hasa kutokea mataifa ya Uchina, Jamhuri ya Korea (Korea ya Kusini) na Marekani ambapo wavumbuzi wa mambo kadha wa kadha, na vitu mbalimbali, walitaka wapatiwe hati ya hakimiliki juu ya uvumbuzi wao.

Hapa na Pale

Baraza la Usalama linatarajiwa kukutana jioni Makao Makuu kupitisha azimio la kuongeza muda wa operesheni za vikosi vya mchanganyiko vya UM/UA kwa Darfur (UNAMID) kufuatilia maridhiano na mataifa ya magaharibi kukubali kuingiza kibwagizo cha pendekezo la nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (UA) kuhusu suala la Mahakama ya ICC ya kutaka kumshitaki Raisi wa Sudan kwa makosa ya jinai ya halaiki katika Darfur. Muda wa awamu iliopita ya shughuli za UNAMID unamalizika saa sita usiku, Alkhamisi, tarehe 31 Julai 2008.~

Radovan Karadzic awekwa rumande Hague kwenye kituo cha UM

Radovan Karadzic Ijumatano asubuhi alihamishwa kutoka Serbia, eneo aliokamatwa mnamo tarehe 21 Julai 2008, na amepelekwa kizuizini mjini Hague, Uholanzi penye Kituo cha Kufungia Watu cha UM. Nerma Jelacic, Msemaji wa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya UM juu ya Yugoslavia ya Zamani (ICTY) alithibitisha taarifa hiyo kwenye mazungumzo na Redio ya UM.~

UM kukomesha ulinzi wa amani mipakani ETHIOPIA/ERITREA

Baraza la Usalama lilikutana mapema asubuhi kuzingatia azimio nambari 1827 (2008) liliopendekezwa na Ubelgiji, la kukomesha shughuli za kulinda amani na uangalizi wa kusitisha mapigano za Shirika la UNMEE mipakani baina ya Ethiopia na Eritrea. Azimio limepitishwa, bila kupingwa na wajumbe wote 15, na limependekeza kusisitisha shughuli za UNMEE kieneo kuanzia Alkhamisi, tarehe 31 Julai 2008.

HAPA NA PALE

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Cote d’Ivoire (UNOCI) limemaliza kuondosha kituo chake cha mwisho cha uangalizi, katika ile sehemu ya nchi inayojulikana kama Eneo la Msitari wa Kijani, eneo liliotenga sehemu ya kusini, iliokuwa chini ya mikono ya vikosi vya serikali, kutoka ile sehemu ya kaskazini ya nchi, ambayo baadhi ya maeneo yake bado yapo chini ya mamlaka ya waasi wa zamani wa kundi la Force Nouvelles. Eneo la Msitari wa Kijani lenye upana wa kilomita 20 na urefu wa kilomita 600, katikati ya Cote d’Ivoire, ni sehemu ya amani iliowekwa makhsusi, na kudhibitiwa na vikosi vya kimataifa, kwa kulingana na mapatano ya amani ya Ougadouguo, kusaidia kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini na kujenga hali ya kuaminiana miongoni mwa makundi yaliokuwa yakikhasimiana.

Ripoti 2008 ya UNAIDS juu ya UKIMWI duniani ni ya mchanganyiko

Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) imewakilisha rasmi hapa Makao Makuu ripoti ya 2008 iliofanya mapitio juu ya maendeleo katika kupiga vita maradhi ya UKIMWI ulimwenguni. Ripoti imesema UNAIDS imekadiria katika 2007 watu milioni 33 ulimwenguni walikuwa wakiishi na virusi vya UKIMWI; na wakati huo huo watu milioni 2.7 waliambukizwa na VVU, na milioni 2 ziada walifariki kwa sababu kadha wa kadha zinazoambatana na UKIMWI.

UNICEF inasema kunyonyesha watoto kunafaidisha afya

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) likijumuika na Shirika la Afya Duniani (WHO) na pia Umoja wa WABA ambao huendeleza miradi ya kimataifa ya unyonyeshaji, wametoa mwito wa pamoja unaopendekeza kuongezwe misaada ya miradi ya kuwahimiza akina mama wazazi wa kimataifa kunyonyesha watoto wao ili kuwakinga watoto wachanga na maambukizo ya magonjwa hatari na maututi ya kitoto.