Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Mataifa ya Kusini na Mashariki mwa Afrika yanaendelea kukabiliwa na mafuriko, ukame na matukio mengine ya mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka ya karibuni
UNDP/Arjen van de Merwe

Tishio la mabadiliko ya tabianchi linaendelea kuongezeka Afrika:WMO Ripoti

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa utabiri wa hali ya hewa WMO ikitanabaisha hali ya sasa na mustakabali wa hali ya hewa katika bara la Afrika inaonyesha kwamba mwaka 2019 ulikuwa miongoni mwa miaka mitatu yenye joto la kupindikia katika historian a mwenendo unatarajiwa kuendelea  ukisababisha watu kutawanywa na athari katika kilimo. 

26 Oktoba 2020

Ripoti yabaini magari mengi yanayopelekwa nchi za uchumi mdogo hayafai. 
Ukosefu wa ajira na makazi salama vyawaacha wafanyakazi wahamiaji hatarini Lebanon, imesema IOM.
Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO huko nchini Madagascar linatekeleza mradi wa kuhakikisha kuwa wakazi wanaoishi karibu na eneo la hifadhi la Makira wanakuwa na uhakika wa kupata mlo bora bila kusambaratisha eneo hilo la hifadhi.
 

Sauti
12'20"
UN

Wakati ni sasa kuchukua hatua kukomesha uchafuzi wa hewa:Guterres

Watu 9 kati ya 10 wanavuta hewa chafu, ni wakati wakubadili hilo sasa Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa kushikamana na kuchukua hatua zinazohitajika dhidi ya hewa chafu inayovutwa na watu 9 kati ya 10 kila uchao duniani kote. Assumpta Massoi na taarifa zaidi

(TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI)

Kupitia ujumbe wake wa maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kimataifa ya hewa safi kwa ajili ya anga ya blu, Guterres ameonya kwamba hewa chafu inayovutwa inachangia kwa kiasi kikubwa magonjwa ya moyo, kiharusi,

Sauti
2'27"

07 SEPTEMBA 2020

Katika Jarida la Habnari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Katika maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kimataifa ya hewa safi kwa ajili ya anga ya rangi ya blu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka mshikamano kutokomeza uchafuzi wa hewa

-Nchini Pakistan mbinu za kupambana na ugonjwa wa Polio zawa mkombozi mkubwa katika vita dhidi ya corona au COVID-19 ikiwemo miundombinu yake

-Waalimu, wanafunzi na wazazi nchini Uganda waelezea changamoto za kusomea nyumbani wakati huu wa janga la corona au COVID-19

Sauti
12'51"
World Bank/Sue Pleming

Hali ya hewa ya Morogoro haikuwa hivi, hatua za pamoja na za haraka zinahitajika-Wakazi wa Morogogo

Mkoa wa Morogogoro ulioko katika eneo la mashariki la Tanzania ni moja ya maeneo ambayo kwa miaka mingi yametambulika kuwa maeneo yenye hali nzuri ya hewa kutokana na mazingira yake kuwa yenye misitu, nyika, na milima yenye kutiririsha maji safi. Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanaharakati wa kutunza mazingira wanaona kuwa ni muhimu kuchukua hatua za kuilinda hali hiyo kwani iko katika hatari ya kutoweka kutokana na shughuli za binadamu kama vile uchomaji mkaa.

Sauti
3'36"

05 Agosti 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Assumpta Massoi 
-Lebanon,iko katika siku ya maombolezo kufuatia mlipuko mkubwa wa jana katika mji mkuu Beirut UNIFIL iko tayari kusaidia.
 - Nchini Niger, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na wadau kutekeleza mbinu za haraka za kukabiliana na utapiamlo uliokithiri miongoni mwa watoto .
- Takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR zinaonesha kuwa theluthi mbili ya raia milioni mbili wa Sudan Kusini wanaoishi uhamishoni, ni watoto.

-Na le

Audio Duration
11'52"