Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 Januari 2021

14 Januari 2021

Pakua

Hii leo jaridani kwa kiasi kikubwa ni masuala ya mabadiliko ya tabianchi tukimulika ripoti ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, kuhusu hatua thabiti za kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kutumia mbinu za asili, halikadhalika ripoti kuhusu viwango vya joto kutoka shirika la hali ya hewa la Umoja wa Mataifa, WMO, ikiutaja mwaka 2020 kuwa moja ya miaka mitatu iliyoongoza kwa kuwa na viwango vya juu sana vya joto duniani. Tunakwenda pia huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambako mapigano mapya yamesababisha vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua. Usisahau makala tunakwenda Ghana kuangazia wazazi waliojitolea kufundisha watoto ili kufanikisha SDGs. Mashinani nako tunamulika SDGs na tuko Somalia. Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'53"