Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi umeishaje, na nini kinafuata?

Mkutano wa 26 wa kimataifa wa mbadiliko ya tabianchi COP26 uliokuwa ufanyike baadaye mwaka huu umehairishwa.
Unsplash/Adam Marikar
Mkutano wa 26 wa kimataifa wa mbadiliko ya tabianchi COP26 uliokuwa ufanyike baadaye mwaka huu umehairishwa.

Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi umeishaje, na nini kinafuata?

Tabianchi na mazingira

Wakuu wa nchi na serikali zaidi ya 70 , wakiwemo pia viongozi wa kikanda, mameya wa miji mbalimbali na wakuu wa mashirika mbalimbali duniani wamewasilisha hatua wanazotarajia kuchukua ili kupunguza kiwango cha hewa chafuzi ya viwandani na kuzuia dunia kuendelea kuchemka na ongezeko la joto katika mkutano wa matamanio ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi uliomalizika Jumamosi jioni.

Miongoni mwa nchi zilizowasilisha mipango yao katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao ni wengi wao ni wale wanaozalisha kiwango kikubwa cha hewa ukaa.
Ahadi zilizotolewa

Uingereza imeahidi kupunguza utoaji wa hewa ukaa kwa asilimia 68 katika kipindi cha miaka mitano ijayo huku Muungano wa Ulaya ukiahidi kupunguza uchafuzi huo kwa asilimia 55. Kipimo cha kuanzia ni kiwango cha uzalishaji wa hewa ukaa ilichokuwepo mwaka 1990.
Angalau nchi 24 zimeongeza kiwango cha ahadi zao ili kuweza kufikia kiwango cha kutozalisha hewa ukaa ifikapo katikati ya karne hii na wengine wamekwenda mbali zaidi, mfano Finland imeahidi kufikia lengo la kutozalisha hewa ukaa ifikapo mwaka 2030, Australia ifikapo 2040 na Sweden ifikapo 2045.
Pakistan kwa upande wake imesema inaachana na ujenzi wa mtambo mpya wa uzalishaji wa makaa yam awe , India imeahidi kwamba muda si mrefu itaongeza mara mbili mipango yake ya matumizi ya nishati jadidifu na China imetoa ahadi ya kuongeza kiwango cha matumizi ya nishati safi zisizo za mafuta ya kisukuku ifikapo mwaka 2030.

Nayo serikali ya Kenya imeahidi kufanya kila liwezekanalo kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa ambao si makubwa kwa kuingia zaidi katika matumizi ya nishati safi ikiwemo ya sola.

Moto wa nyika ukiteketeza eneo huko California Marekani mwaka 2018
Peter Buschmann for Forest Service
USDA
Moto wa nyika ukiteketeza eneo huko California Marekani mwaka 2018


Nini kinachofuata

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ambao ni moja wa waandaji wa mkutano huo, mkutano wa jana ni mwanzo wa maandalizi ya mkutano wa pande za mkakati wa mkataba wa umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi au COP26.
Mkutano huo ilikuwa ufanyike mwezi huu wa Desemba mjini Glasgow Uingereza lakini kutokana na janga la COVID-19 mkutano ikabidi uhairishwe hadi mwakani.
Lakini ni kwa nini ni muhimu: chini ya masharti ya makubaliano ya mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi washiriki wake wanatakiwa kila baada ya miaka mitano kutathimini mipango yayo ya kitaifa ya hiyari katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa mwelekeo wa kuongeza ahadi zao na kuziwasilisha rasmi katika mkutano wa mwisho wa mwaka ambao washiriki sio tu wanachama wa mkataba huo bali pia wataalam, wawakilishi wa makampouni ya biashara , asasi za kiraia, wanazuoni na wanaharakati wanashiriki.

Watoto wakitembea katika maji ya mafuriko katika jimbo la Jonglei, Sudan Kusini.
© WFP/Musa Mahadi
Watoto wakitembea katika maji ya mafuriko katika jimbo la Jonglei, Sudan Kusini.


Daraja la kuelekea COP-26

Hivyo kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mkutano huu wa matamanio ni daraja la kuvuka kuingia kwenye COP-26 na pia umezitia msukumu zaidi nchi kuchukua maamuzi bora zaidi yah atua za kufikia lengo la kutozalisha hewa ukaa ifikapo mwaka 2050.
Na lengo hilo ni muhimu katika kuhakikisha joto la dunia haliongezeki Zaidi ya nyuzijoto 1.5C ambalo ni moja ya malengo ya mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi, na wanasayansi wameonya kwamba endapo hili halitotokea basi dunia itakabiliwa na zahma kubwa ya ongezeko la joto duniani ambalo athari zake hazielezeki.
Guterres amesema “Janga la COVID-19 limedhoofisha uchumi wa dunia lakini maendeleo ya upatikanaji wa chanjo yanatoa tumaini kwamba uchumi huo utaweza kuimarika tena hivi karibuni na mambo kuweza kurejea katika hali ya kawaida. Binadamu lazima waitumie fursa hii kuanza safari ya kuwa na uchumi unaozingatia mazingira na usiozalisha hewa ukaa.”