Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

22 APRILI 2020

Leo katika jarida la Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea

-Umoja wa Mataifa unasema janga la virusi vya Corona au COVID-19 ni kengele ya kuiamsha dunia kuchukua hatua kulinda sayari hiyo na watu wake  hasa leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya mama sayari dunia

- Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na jiji la Nairobi wanachukua hatua kudhibiti kusambaa wa virusi vya corona au COVID-19, kwenye makazi dunia ya Kibera.

Sauti
12'44"

20 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Flora ucha kutoka Umoja wa Mataifa anakuletea

- Serikali ya Tanzania yaitikia wito wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO na leo imezindua mkakati wa ufundishaji kupitia teknolojia ya Radio na Televisheni kuhakikisha watoto wanasoma wakati huu wa COVID-19

- Mabalozi wema wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD Idris Elba na mkewe sabrina Elba leo wamezindua mfuko na ombi la dola milioni 200 kuwasaidia wakulima vijijini wakati huu wa janga la Corona ili kuhakikisha uhakika wa chakula

Sauti
13'24"
UN News/Assumpta Massoi

Mabadiliko ya tabianchi Pangani, Tanga ni dhahiri- Afisa Mifugo

Kadri siku zinavyosonga hivi sasa, shughuli za binadamu zinavyoshamiri, vivyo hivyo mabadiliko ya tabianchi ambayo nayo yanazidi kuwa dhahiri miongoni mwa wakazi wa maeneo mbalimbali. Kila sekta imeguswa. Hali inakuwa ni changamoto zaidi kwa wakazi walio karibu na fukwe au wanaopakana na bahari. Mathalani nchini Tanzania kwa wakazi wa Pangani mkoani Tanga shughuli za kilimo,uvuvi na ufugaji zimeathirika na wanapaswa kuchukua hatua zaidi. Je madhara ni kwa kiasi gani?

Sauti
4'26"
UN News/Assumpta Massoi

FAO imetuepusha na kilimo cha mazoea- Wanawake Kakonko

Mkoani Kigoma nchini Tanzania hususan katika kata ya Katanga wilayani Kakonko, ushirikiano kati ya serikali na Umoja wa Mataifa kwenye kuhakikisha wakulima wanahimili mabadiliko ya tabianchi umeanza kuzaa matunda. Ushirikiano huo unaosongeshwa na wananchi wenyewe kwa ubia na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO ni katika kuwapatia wakulima mbinu bora za kilimo ili kuwepo na uhakika wa chakula.

Sauti
4'17"
UNHCR/Zinyange Auntony

Mwaka mmoja baadaye, kimbunga Idai bado ni jinamizi kwa manusura wake

Mwaka mmoja tangu kimbunga Idai kipige eneo la kati la Msumbiji idadi kubwa ya manusura ya janga hilo bado wameshindwa k urejea katika maisha ya kawaida kutokana na uhaba wa fedha za ukarabati. 

Kimbunga Idai kilipiga mji wa Beira katika jimbo la Sofala katikati mwa Msumbiji usiku wa Machi 14 na 15 ambapo kabla ya hapo kulishuhudiwa mvua kubwa na mafuriko katika nchi tatu ikiwemo Msumbiji, Zimbabwe na Malawi na kusababisha maelfu ya watu kufurushwa makwao na vifo na uharibifu wa mali.

Sauti
2'3"

10 Machi 2020

Kuna ongezeko la ishara na madhara ya mabadiliko ya tabianchi katika anga, ardhi na baharini yasema ripoti ya WMO. Programu ya kupatia wakimbizi wa Syria fedha Uturuki yawa nguzo ya maisha yao. MINUSCA yawapatia wanawake wafungwa CAR mafunzo ya ujasiriamali. Makala tunabisha hodi mkoani Dodoma nchini Tanzania na mashinani tupo nchini Kenya. Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Sauti
10'26"
WMO/Vladimir Tadic

Ripoti mpya yaonesha kuna ongezeko la ishara na madhara ya mabadiliko ya tabianchi katika anga, ardhi na baharini

Ishara za mabadiliko ya tabianchi kama vile ongezeko la joto la ardhini na baharini, kuongezeka kwa kina cha bahari na kuyeyuka kwa barafu, vimeangaziwa katika ripoti mpya ya Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO na wadau wake iliyotolewa hii leo Machi 10 mjini New York Marekani na Geneva Uswisi. 

Ripoti hiyo imeeleza madhara ya matukio ya hali ya hewa na tabianchi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, afya ya binadamu, uhamiaji na ukosefu wa makazi, uhakika wa chakula, ardhi na maisha ya viumbe vya majini.

Sauti
2'29"